Unknown Unknown Author
Title: RAIS KIKWETE:SERIKARI HAITA ANZISHA MAHAKAMA YA KADHI!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Rais Kikwete amesema serikali haiwezi kuanzisha wala kuiendesha na kuihudumia Mahakama ya Kadhi na ameongeza kuwa hilo ni jukumu la Waislam...

Rais Kikwete amesema serikali haiwezi kuanzisha wala kuiendesha na kuihudumia Mahakama ya Kadhi na ameongeza kuwa hilo ni jukumu la Waislamu wenyewe na kwamba hawazuiliwi kuianzisha Mahakama hiyo na kwamba hayo ndio yalikuwa makubaliano.

Pia,Raisi Kikwete amesema tamko la viongozi wa dini kuhusu swala la katiba mpya, limemshangaza, limemfedhehesha na kumsikitisha sana.

Raisi Kikwete ameyasema hayo katika kikao cha kamati ya amani cha viongozi wa dini wa mkoa wa Dar-es-salaam.

Chanzo:ITV

SOMA ZAIDI:
Mh.Rais Prof Kanali Jakaya Mrisho Kikwete amesema swala la mkanganyiko wa mahakama ya kadhi linatokana na uelewa mdogo wa wananchi juu ya swala hili,Rais amesema si jukumu la Serikali kuisimamia na kuiendesha Mahakama ya Kadhi, bali ni jukumu la Waislam wenyewe.


Rais Kikwete ameongea hayo leo jijini Dsm alipokutana na "Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Dsm" inayojumuisha viongozi wa dini mbalimbali,JK amesema serikali inachoweza kuwasaidia Waislam ni kuupeleka mswaada bungeni ili baadhi ya taratibu na sheria zake zake zinazofaa zitambuliwe rasmi ndani ya nchi na si kuiendesha na kuighalamia kwa kuwalipa makadhi watakaoiendesha mahakama hiyo,amewaasa waislam kuojiandaa kuighalamia mahakama hiyo,kwani serikali I tayari imetimiza wajibu wake wa kuuopeleka mswaada wa mahakama hiyo bungeni ili uundiwe she ria kamili.


Pia JK ametumia nafasi hiyo kuwaasa viongozi wa dini kuungana na serikali kuelimisha watu juu ya katiba mpya,na sio kutoa matamko yenye lengo la kuwagawa wananchi kwa misingi ya imani zao, amewaambia Viongozi hao kasikitishwa na matamko ya viongozi wa dini juu ya kuipigia kura ya "HAPANA" rasimu ya Katiba inayopendekezwa.


Wakati huohuo Mkuu wa mkoa wa DSM Mecky Sadick amewataka viongozi wa kidini kutoishia kuwakemea waumini wao tu,bali na viongozi wenzao wa dini ambao wanatoa matamko kwa waumuni wao yenye lengo la kuleta viashairia vya uvunjifu wa amani na mshikamano wa nchi.



MJUMBE BLOG
Tunashukuru kwa kutupa ridhaa ya kukuhudumia.



Hjhjj



Bhjjj

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top