Unknown Unknown Author
Title: REKODI YA MAKOCHA NA VIKOMBE WALIVYOBEBA BARANI ULAYA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Hapa nawaletea wastani wa makocha maarufu barani Ulaya jinsi walivyochukua makombe, Mtaona idadi ya mechi ambazo makocha hao maarufu huw...




Hapa nawaletea wastani wa makocha maarufu barani Ulaya jinsi walivyochukua makombe, Mtaona idadi ya mechi ambazo makocha hao maarufu huwa wanahitaji kuchukua Kombe moja, Kwenye orodha hii, pia wapo makocha wakongwe na wastaafu na wengine waliokwisha fariki.

1] JOSE MOURINHO;
Baada ya kushinda Kombe la Ligi jumapili dhidi ya Tottenham Hotspurs, sasa Jose Mourinho ana wastani wa kupata kombe moja kila baada ya mechi 35 kila anakofundisha, Ameshafundisha mechi 727 na ana makombe 21 jumla.

2] PEP GUARDIOLA;
Huyu jamaa ndie kiboko ya makocha wote barani Ulaya kwa wastani wa mechi zake na idadi ya makombe aliochukua ndani ya muda mfupi.
Amefundisha mechi chache mpaka sasa na wastani wake wa kuchukua kombe baada ya mechi kadhaa ni mzuri sana na unavutia kuliko kocha yeyote barani Ulaya.

Pengine hilo linaweza kuwa linamuumiza Mourinho ambaye ni hasimu wake mkubwa Baada ya Guardiola kufundisha mechi 378 na kufanikiwa kubeba makombe 19, huku akiwa na wastani wa kuchukua Kombe kila baada ya mechi 19.89 karibia 20 tuseme.

3] BOB PAISLEY;
Kafundisha mechi 535 na amechukua makombe 20, wastani wake ni kuwa anapata Kombe kila baada ya mechi 26.75.

Huyu alifundisha timu moja tu. Aliifundisha Liverpool tu. Anajulikana kama “Mr Liverpool”. Aliitumikia Liverpool akiwa kama mchezaji, mtaalamu wa mazoezi ya viungo vya mwili, kocha na kisha kocha mkuu wa timu hiyo kati ya 1939 na 1983.

Wakati akiwa Kocha mkuu wa timu hiyo miaka kati ya 70 na 80, ulikuwa ni wa mafanikio ya ajabu, ambapo Liverpool walishinda makombe sita ya Ligi Kuu, makombe matatu ya Kombe la Ligi, na makombe matatu barani Ulaya kati miongoni mwa makombe alioshinda.

Hiyo inamaanisha kuwa Liverpool walikuwa wanashinda Kombe moja kila baada ya mechi 26 wakati wa uongozi wake.

4] WALTER SMITH;
Mechi 766, makombe 21, wastani wa mechi 36.47.

Kwenye vipindi viwili akiwa uongozini kama kocha, Smith alijenga na kuimarisha utawala wa Glasgow Rangers kwenye soka la nchini Scotland, akiwaongoza kuchukua makombe 10 ya Ligi Kuu, makombe matano mengine na makombe sita ya Kombe la Ligi nchini humo.

Alikuwa kocha msaidizi wa Rangers kuanzia mwaka 1986 hadi 1991 ambapo sasa mwaka 1991 ndio akapewa jukumua la kuifundisha timu akiwa kama kocha mkuu akirithi nafasi ya Graeme Souness (mkongwe wa Liverpool). Kabla ya kuwa kocha msaidizi wa Rangers, alikuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Scotland akimsaidia Alex Ferguson kwenye Kombe la Dunia mwaka 1986 nchini Mexico.

Aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa Rangers 1991 na alikaa kwenye timu hiyo hadi mwaka 1998. Kwa kipindi hicho cha miaka 7 akiwa ndie kocha wao, alichukua makombe 13 jumla ambapo ndani yake kuna makombe 7 mfululizo ya Ligi Kuu alioshinda.

Baada ya hapo akaenda kuifundisha Everton kwa misimu minne kutoka mwaka 1998 hadi 2002 na hapo akatimuliwa.

Akawa kocha wa timu ya taifa ya Scotlanda mwaka 2004 na Januari 2007 akarudi tena Rangers mpaka 2011. Alishinda makombe nane jumla kwenye kipindi chake hiki cha pili na aliiongoza timu hiyo hadi kwenye fainali ya Kombe la UEFA (Europa League) mwaka 2008.

Huyu ndie kocha anayeshika nafasi ya pili kwa mafanikio kwenye timu hiyo baada ya Bill Struth.

5] JOCK STEIN;
Mechi 1005, makombe 27, wastani wa kuchukua Kombe ni kila baada ya mechi 37.

Wakati mashabiki wa Rangers wakisherehekea mafanikio ya Smith, wapinzani wao wakubwa kwenye Ligi hiyo, Celtic, wao watamshukuru milele Jock Stein kwa kuwafanya watawale miaka 60 na 70.

6] OTTMAR HITZFELD;
Mechi 1039, makombe 26, wastani wa Kombe kila baada ya mechi 39.96 karibia 40.

7] LOUIS VAN GAAL;
Mechi 831, makombe 19, Kombe kila baada ya mechi 43.73 karibia 44.

8] VICENTE DEL BOSQUE;
Mechi 472, makombe 10, Kombe kila baada ya mechi 47.2.

9] FABIO CAPELLO;
Mechi 625, makombe 13, Kombe kila baada ya mechi 48.07.

10] ROBERTO MANCINI;
Mechi 627, makombe 13, Kombe kila baada ya mechi 48.23.

11] SIR ALEX FERGUSON;
Mechi 2131, makombe 44, Kombe kila baada ya mechi 48.43.

Kwa mbali huyu ndie kocha mwenye mafanikio zaidi kwenye orodha hii na ndie aliefundisha kwa muda mrefu zaidi.

Mafanikio yake yalianzia St Mirren mwaka 1977, kabla ya kwenda Aberdeen miaka ya 80 mwanzoni na kuchukua Kombe la Washindi barani Ulaya mwaka 1983.

Lakini wote tunajua kuwa mafanikio yake ameyapata zaidi akiwa Manchester United, ambapo alishinda makombe 13 ya Ligi Kuu, makombe matano ya Kombe la FA, makombe manne ya Kombe la Ligi, makombe mawili ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, na makombe mawili ya Washindi barani Ulaya.

12] MARCELO LIPPI;
Mechi 958, makombe 19, Kombe kila baada ya mechi 50.42.

13] CARLO ANCELOTTI;
Mechi 952, makombe 16, Kombe kila baada 59.5

14] RAFAEL BENITEZ;
Mechi 912, makombe 12, Kombe kila baada ya mechi 76.

15] ARSENE WENGER;
Mechi 1487, makombe 17, Kombe kila baada ya mechi 87.47.

16] BRIAN CLOUGH;
Mechi 1319, makombe 13, Kombe kila baada ya mechi 101.46.

17] BILL SHANKLY;
Mechi 1160, makombe 11, Kombe kila baada ya mechi 105.45.

18] SIR BOBBY ROBSON;
Mechi 1446, makombe 13, Kombe kila baada ya mechi 111.23.

   CHANZO:SHAFFIH DAUDA

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top