Sehemu ndogo ya shehena ya mahindi yaliyonunuliwa na serikali na kuhifadhiwa nje ya maghara ya NFRA, Vwawa Mbozi baada ya maghala kujaa, Machi 1, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe, mama Tunu wakikagua sehemu ya shehena ya mahindi iliyohifadhiwa nje ya maghala ya Hifadhi ya Taifa ya Chakula, NFRA, enjeo la Vwawa, wilayani Mbozi mkoani Mbeya Jumapili Machi 1, 2015. Maelfu ya tani ya mahindi, yamelazimika kuhifadhiwa nje baada ya maghala yaliyotengwa maalum kuhifadhi nafaka hiyo kujaa.
Kilio cha wananchi wengi nchini kimekua ni UBINYU wa soko la mazao yao...
Kila kona wananchi walio wekeza kwenye zao la mahindi wame lalamikia bei kuwa isiyo endana na gharama za uendeshaji wa kilimo.
Kilio hicho kimeshuhudiwa na Mhe.Mizengo Pinda pia katika ziara yake Mkoani mbeya hivi majuzi alipo shuhudia mlima wa shehena ya Mahindi ukiwa Ume kosa hata hifadhi.
Kuna pande mbili hapa;
Upande wa TANZANIA kama taifa kujivunia utajiri wa mavuno ya kutosha kupambana na njaa.
Lakini upande wa Changamoto za kiutendaji na Uhaba wa soko la uhakika kwa wakulima wa zao husika ambalo lime endelea kuwa didimiza wakulima wadogo na kuwa inua mawakala na madalali wa kilimo.
Hapo ndipo ilipo Changamoto?
Tufanyeje basi?
Hili ni suala la kimfumo na huwezi tengeneza jibu au hitimisho moja bali kuna hitaji upembuzi wa kina kabla hajatafutwa wa kutupiwa lawama.
Ni imani yetu;Shehena ya mahindi wilayani mbozi,imetoa ujumbe kwa wahusika..."
MJUMBE BLOG
Tunashukuru kwa kutupa fursa ya kukuhudimia.
Karibu tena ututembelee.
Post a Comment