EMT 04:05 Yesterday
Wakati watu wengi wakiwa wamejikita kwenye ile miswada iliyokuwa iletwe bungeni kwa hati dharura, wiki iliyopita, serikali ilitumia mwanya huo kuleta Bungeni na wabunge kupitisha Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2014. Sheria hii ina karibu vifungu 40, lakini kifungu muhimu zaidi ni kile cha 37 ambacho kinaweka makosa na adhabu zinazohusiana na uchapishaji wa takwimu ambazo siyo za, au hazijaidhinishwa na, Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
Kwanza, kifungu cha 37(1)(b) kinasema kuwa mtu yeyote ambaye bila ya mamlaka halali, atachapisha au kutoa kwa mtu mwingine yeyote taarifa alizozipata kwa mujibu wa kazi yake kinyume na utaratibu wa kawaida wa ajiraatakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atahukumiwa faini isiyopungua milioni mbili au kifungo cha muda usiopungua miezi sita, au vyote kwa pamoja.
Pili, kifungu cha 37(1)(c) kinasema kuwa mtu yeyote ambaye anatelekeza jukumu lake au kwa makusudi atatoa tamko lolote, kauli au rejesho katika utekelezaji wa kazi yake, au anakusanya na kuzitoa taarifa zozote za uongo za takwimu atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atahukumiwa faini isiyopungua milioni mbili au kifungo cha muda usiopungua miezi sita, au vyote kwa pamoja.
Tatu, kifungu cha 37(2) kinasema kuwa mtu yeyote ambaye anamiliki taarifa yoyote ya kitakwimu, ambayo kwa ufahamu wake anajua zimetolewa kinyume na masharti ya sheria hii, anachapisha au anasambaza kwa watu wengine taarifa hizo, anatenda kosa, na akipatikana na hatia atahukumiwa faini isiyopungua shilingi milioni tano au kifungo cha muda usiopungua miezi kumi na mbili, au vyote kwa pamoja.
Nne, Kifungu cha 37(4) kinasema kuwa chombo chochote cha habari ambacho kitachapisha taarifa za kitakwimu za uongo au za upotoshaji, au kutangaza kipindi chochote kinachohusu shughuli za ukusanywaji wa taarifa ambayo imefanywa au inafanywa na Ofisi, na hatimaye kusababisha wananchi wasishiriki kwenye shughuli hiyo ya ukusanywaji wa taarifa au wasishirikiane na maafisa wa Ofisi, kinatenda kosa na kitakapotiwa hatiani kitawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni kumi au kifungo cha muda usiopungua miezi kumi na mbili au vyote
viwili.
Tano, Kifungu cha 37(5) kinasema kuwa mtu yeyote au wakala ambaye, bila idhini ya kisheria kutoka kwa Ofisi, atachapisha au kusambaza taarifa za kitakwimu ambazo zinaweza kusababisha upotoshwaji wa taarifa husika, atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatakiwa kulipa faini isiyopungua shilingi milioni kumi au kifungo cha muda usiopungua miaka miezi ishirini na nne.
Mwisho, kifungu cha 37(6) kinasema kuwa kwa madhumuni ya kifungu chote cha 37, “chombo cha habari” kinajumuisha kituo cha radio, kituo cha televisheni, gazeti au jarida, tovuti au chombo kingine chochote cha habari.
Moja ya madhumuni mazuri ya sheria hii mpya ni kupambana na "data za kupika", "wapika data" na labda "viwanda vya kutengeneza uongo". Kwa mujibu wa kitabu Karim Hirji: Statistics in the Media: Learning from Practice (Media Council of Tanzania, 2012), kumekuwa na ongezeko la takwimu ambazo nyingine ni za kupika. Baadhi ya waandishi wa habari, watafiri na maafisa wa serikali wamekuwa wakiudanganya umma kwa takwimu za kupiga au za upande mmoja. Kwa hiyo, wapika data na wale wenye viwanda vya uongo wajiandae.
Hata hivyo, inadaiwa kuwa sheria hii imeenda mbali mno kiasi cha inaweza kuifanya Tanzania kuwa mahali pagumu kwa mashirika ya uchapishaji, watafiti na wasomi kufanya kazi kwa sababu sheria hii inadhibiti uchapishaji wa takwimu zozote ispokuwa zile ambazo zimechapishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kuweka adhabu kali kwa yoyote yule atakayeenda kinyume na sheria hii.
Mfano, Karim Hirji anadai kuwa sheria hiyo itaifanya Tanzania irudi kwenye zama za utawala wa kifalme kuhusiana na usambazaji wa habari. Enzi hizo huko Ulaya wanasayansi walikuwa wananyongwa kwa kuchapisha takwimu zilizokuwa zinapingana na zile za watawala. Anasema siku hizo zimepitwa na wakati na sheria za aina hii haziko tena kwenye vitabu vya sheria, maana hata kipindi cha Hitler na Nazi, ubaguzi wa rangi Afrika ya Kusini na wakati wa ukoloni ambapo ukandamizaji mkubwa wa hoja mbadala na uhuru wa habari vilikuwa vimeshika hatamu, kulikuwa hakuna sheria za takwimu.
Inadaiwa kuwa sheria hii mpya itaathiri kwa kiasi kikubwa taasisi za elimu kwa sababu kwa kuifanya Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuwa taasisi pekee ya kuidhinisha takwimu kutapunguza uhuru na tafiti nyingine kukosoa takwimu za Ofisi hiyo. Inadaiwa taasisi za utafiti na elimu nafasi na uhuru wa kufanya kazi zake, ambazo nyingi ni muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Sheria hiyo inadaiwa kupingana haki na uhuru raia na makundi mbalimbali ya wadau kupata au kukusanya taarifa muhimu zinazohusiana na maisha ya Mtanzania wa kawaida kama takwimu za upungufu wa vyoo katika shule zilizopo mkoa fulani, kiasi cha utapiamlo kwenye eneo fulani (Tanzania ni ya tatu kwa utampiamlo Afrika), matumizi mabaya ya bajeti za wizara, rushwa, nk. Mtafiti, mwandishi wa habari, au mdau yoyoe yule hataweza kukusanya au kuchapisha taarifa hizi muhimu bila idhini ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
Pia inadaiwa sheria hii imelenga kuzia hoja na takwimu mbadala hasa katika mwaka huu wa uchaguzi. Kwa mfano, Machi mwaka huu Ofisi ya Taifa ya Takwimu ikishirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar imeandaa taarifa kuhusiana na makadirio ya idadi ya watu na wapiga kura kwa mwaka 2015. Idadi hiyo imetolewa katika ngazi ya Taifa, Mkoa, Wilaya, Jimbo na Kata kwa mujibu wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012. Taarifa hiyo inakadiria idadi ya wapiga kura kwa mwaka 2015 kuwa 24,253,541. Kwa hiyo, mtu mwingine akija na makadirio tofauti na ambayo hayajaidhinishwa na Ofisi hiyo anaweza akawa ameenda kinyume na sheria hii mpya.
Kama Rais Kikwete atatia saini Sheria ya Takwimu, basi vyombo vya habari, waandishi wa habari, makampuni ya uchapishaji na taasisi za elimu na utafiti vitatakiwa kuripoti takwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu tuu au data ambazo tayari zimeshaidhinishwa na Ofisi hiyo. Pia sheria hiyo itakuwa inaenda kinyume na ‘Open Government Initiative” ambayo Rais Kikwete ameishikia bango katika kipindi cha utawala wake.
MAELEZO ZAIDI:
MCHANGIAJI MWINGINE:
Vipi kama badala ya ku-refer data za World Bank ukaamua kufanya utafiti wako mwenyewe, let's empirical research kwa kukusanya evidence through experimentation or observation na kuzichapisha?
Halafu uzuri au ubaya wa tafiti huwezi kuja na majibu yanayofanana. Kama alivyosema Hirji watafiti huwa wanatofautiana na wanaweza kufikia conclusions tofauti kwa kutumia data hizo hizo.
Kwa maana hiyo how can we say that takwimu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu au hata za World Bank kuwa GDP ya Tanzania ni 2bn$ are absolute truth?
Ukifaya tafiti zako mwenyewe na kusema kuwa Tanzania ina population ya watu milioni moja, na uka-prove hivyo, huna makosa.
The keyword is distortion of facts, yaani lazima data ziwe za kweli. Ukisema Tanzania kuna wachawi 90%, itabidi NBS wakuprove wrong ndio uwe na makosa.
MCHANGIAJI MWINGINE:
'...The keyword is ditortionof facts, yaani lazima data ziwe za kweli.
Tunarudi kule kule kuwa huwezi kudhibitisha kuwa certain data are absolute true.
Data nyingine ni sampling tuu and do not accurately reflect the population studied.
Kwa mfano, kwa mujibu wa takwimu za NBS idadi ya wapiga kura kwa mwaka 2015 inadiriwa kuwa 24,253,541.
How can you say that hizi data ni za kweli taking into account that science and social analysis has no divine truths?...'
Credit:Jf
MJUMBE BLOG
Kwa picha,Matukio,Taarifa,Habari kila mara.
Post a Comment