UFISADI KWENYE MAJENGO YA TAASISI ZA UMMA MBOZI!
Pichani ni moja ya Majengo ya Umma likiwa lime egeshewa Miti ili kulinusuru lisidondoke,Wilayani Mbozi(Jina la Mahali husika Lina Hifadhiwa).
Hii ni aibu....
Fedha ya Umma inapo geuzwa Posho ya kulipana na Mashemeji zako kwenye kikao cha ukoo...
Nili hamaki sana nilipo kutana na Kioja hiki!
Kioja cha Jengo moja la umma Kuegeshewa miti ili lisi poromoke!
Jengo ambalo lilijengwa kwa madhumuni ya kuhudumia umma kwenye Taasisi hiyo.
Ninge kuwa Tukuyu Basi ninge sema wenzetu hawa Wame buni Mtindo kutoka Kuegesha Mgomba Ulio zidiwa na Mkungu hata kujenga Nyumba yenye Matege...
Nijengo ambalo lilikuwa Limesha ezekwa Wilayani Mbozi,Mbeya huku likiwa na Nyufa kadhaa na Kuegeshewa Miti Lisi anguke...
Tenda ame pewa Mkandarasi,Mhasibu au Mkaguzi?
Na kama ni Mkandarasi,Mkaguzi alipewa mgawo?
Kwa Mtanzania anaye ona jinsi Kodi zetu zinavyo fujwa na watu walio pewa dhamana UTAMSHAWISHI Vipi awe mwaminifu kwa kujitoelea KIPATO chake,MUDA wake na NGUVU zake ili kufanikisha dhamira ya Ujenzi wa Majengo ya Umma!
Majengo ambayo baada ya Miaka miwili yana anza Kutegeshewa Miti ili yasi anguke kama Mgomba au Magofu ya Mji Mkongwe?
Wahusika Fedha Wame weka Mfukoni;Ikidondokea jamaa an Ndugu zetu Tuna iita ni MIPANGO YA MUNGU...
Mipango ya MAFISADI ina batizwa jina zuri...!
Ni fedheha kwa macho yaonayo haya na yaka yachelea,
Ni fedheha kwa Umma uwapao dhamana viongozi kama hawa...
Ni fedheha kwa wana Mbozi pia!!
MBOZI IME GEUZWA PANGO LA WACHUMIA TUMBO...
Na miundo mbinu ya Reja reja kama wilaya iliyo katika Mipango ya mpito...
Wilaya inayo subiri Kuhamishiwa eneo flani...
NI AIBU YETU kama WATANZANIA PIA.
Najua wengi Watauliza lipo Mbozi wapi? Ni Jengo la nini?
Mbozi ni Mbozi tu...
Kwani Wanapo Tumia RUZUKU na KODI zetu huwa hawa ulizi za Mbozi Mashariki au Magharibi?
Picha ya Jengo ilichukuliwa Mbozi mwaka 2014,Juni.
Ime wekwa Humu kwa Hisani ya MAKTABA ZA MJUMBE BLOG.
Asante ya picha MTEMBEA BURE,wa MJUMBE BLOG.
MJUMBE BLOG
Tuna shukuru kwa kutupa fursa ya kuku hudumia.
Karibu tena.
Post a Comment