Siku chache baada ya waziri wa ardhi nyumba na makazi William Lukuvi kutembelea wilaya ya Arumeru kwa lengo la kutatua migogoro ya ardhi usiku wa kuamikia leo watu wasiyo julikana kutoka vijiji vya Ndatu na Kwaranka wamebandika mabango kuzunguka shamba la mwekezaji la Karamu Cofee Estate yakiwa na ujumbe mbalimbali zikimtaka alikabidhi kwa wananchi ndani ya siku saba vinginevyo watavamia kufeka kilichomo na kugawana kwakuwa halitumiki huku wananchi wakikosa ardhi ya kilimo.
ITV ilifika katika shamba ilo na kushuhudia mabango yenye ujumbe tofauti kuzunguka shamba ilo huku wakazi wa vijiji hivyo wakiilaum serikali kuwapatia wawekezaji maeneo makubwa wasiyo na kazi nayo na kuwaacha wananchi bila kitu na kukosa hata eneo la kujenga zahanati na shule hali inayochangia kuchochea migogoro.
Mwenyekiti wa kijiji cha Nkwaranga Zephania Mwanuo amesema kwa muda mrefu uongozi wa vijiji hivyo umejaribu kutuliza wananchi wasifanye vurugu na kupeleka suala ilo kwa uongozi wa serikali lakini wamekosa ushirikiano.
Mbunge wa Arumeru mashashariki Joshua Nasari amesema umefika wakati wa serikali kufanya juhudi za kutatua migogoro katika wilaya ya Arumeru ambayo sehemu kubwa ya ardhi yake inamilikiwa na wawekezaji ambao wameanza kuiuza kwa matajiri na kuongeza migogoro inayoghalimu uhai wa binadamu
Na:Daniel kilonge;ITV.
Post a Comment