Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amewasili mkoani Arusha kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa wawekezaji vijana unaohudhuriwa na wajumbe zaidi ya 400 kutoka mataifa mbalimbali duniani asilimia kubwa wakiwa ni vijana.
Mh.Mugabe ambaye pia ni mwenyekiti wa umoja wa nchi za afrika alipowasili katika uwanja wa ndege wa kilimanjaro alipokelewa na ujumbe wa viongozi wa na watendaji mbalimbali akiwemo makamu wa rais Dr. Mohamed Gharibu Bilal na katibu mkuu wa CCM Bw.Abdulrahamani Kinana.
Muda mfupi baada ya kuwasili kwa MH.Rais Mugabe majira ya saa nane mchana akafuatiwa na Mh.Rais Dr.Jakaya Kikwete na baada ya mapokezi woliongozana hadi katika hotel ya Ngurdoto na kufanya mazungumzo ya faragha kabla ya kwenda kwenye ukumbi wa mkutano
Wakati viongozi hao wakipokelewa katika uwanja huo wa ndege wa kilimanjaro wajumbe wengine waliokwishawasili kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo china walikuwa wakiendelea na vikao vya utangulizi wa mkutano huo katika Hotel ya Ngurdoto
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo Bw.Steven Masele amesema wageni wote walioalikwa wameshafika wakiwemo wawekezaji vijana wa katika sekta ya madini zaidi 150 kutoka china ambao wanatarajiwa kukutana na kubadilishana uzoefu na wawekezaji wa Tanzania.
Cred
Post a Comment