Unknown Unknown Author
Title: Hivi ndivyo RIDHIWANI KIKWETE AMEWASTIRI WAJAWAZITO!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Diwani wa kata ya Kimange Hussein Hadingoka kushoto akipokea fedha kiasi cha shilingi milioni moja toka kwa katibu wa Mbunge wa Chalinze Id...

Diwani wa kata ya Kimange Hussein Hadingoka kushoto akipokea fedha kiasi cha shilingi milioni moja toka kwa katibu wa Mbunge wa Chalinze Iddy Swala kwa niaba ya Mbunge kwa ajili ya ofisi ya kata fedha zilizotolewa na Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete.

Na John Gagarini, Chalinze

ADHA ya akinamama wajawazito kujifungua mbele za wanaume kutokana na zahanati ya Kijiji cha Pongwe Kiona wilayani Bagamoyo mkoani Pwani kuwa na chumba kimoja cha matibabu huenda ikaondoka baada ya kuchangiwa kiasi cha shilingi milioni moja na mifuko 70 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wanawake na wanaume.

Kutokana na zahanati hiyo kuwa na chumba kimoja imesababisha akinamama kujifungua huku kukiwa na wanaume jambo ambalo limesababisha kutokuwa na usiri hivyo utu wa mwanamke kutokuwepo. Msaada huo umetolewa na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ambapo fedha na Saruji vilikabidhiwa na Katibu wa Mbunge huyo Iddy Swala kwa niaba ya Mbunge.

Akizungumzia changamoto hiyo mwenyekiti wa kijiji hicho Rajab Mgaya alisema kuwa zahanati hiyo ilijengwa mwaka 1964 na ina wodi moja tu.

“Tunamshukuru Mbunge kwani hii ilikuwa changamoto kubwa kwa akinamama wanaojifungua huku kukiwa na akinababa nao wanapata matibabu humo hivyo usiri kutokuwepo kutokana na hali hiyo,” alisema Mgaya. Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kimange Husein Hadingoka alisema kuwa mbunge huyo ameonyesha upendo wa hali ya juu kwa kutoa vitu hivyo ambavyo vitasaidia ujenzi huo.

Hadingoka alisema kuwa wananchi watafanya ujenzi huo ambapo yeye alitoa 100,000 kwa ajili ya kufanikisha ujenzi huo na kusema atafurahi kuona uujenzi huo unakamilika mapema.

Naye moja ya wakazi wa Kijiji hicho ambaye ni mwanamama Sikudhani Ally alisema kuwa kujifungua huku wanaume wakiwepo ni mtihani mkubwa lakini kwa mpango huo utakuwa umeweka stara ya mwanamke.

Kwa upande wake katibu wa Mbunge Swala alisema kuwa mbunge ametoa msaada huo baada ya kutemebelea hivi karibuni akiwa kwenye ziara zake za kikazi na wananchi kutoa kilio chao juu ya hali hiyo.
Credit:Issa Michuzi

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top