Baraza la Madiwani Mbozi
Katika kikao cha baraza la Madiwani kilicho fanyika siku ya Alhamis 21 May 2015.
Moja ya agenda ya kikao hicho cha baraza la madiwani ilikuwa ni kuligawa jimbo la mbozi mashariki katika majimbo mawili.
Majimbo yaliyo kuwa yame pendekezwa ni Jimbo la Mbozi na Jimbo la Igamba kwa mchanganuo ufuatao kama ulivyo tolewa na Mtoa habari wetu;
Jimbo la Igamba lina kata zifuatazo:Nambinzo;Itaka,Bara,Halungu,Msia,Wasa,Magamba,Isansa,Itumpi,Igamba,Shiwinga,Mlowo na Myovizi.
Jimbo la Mbozi lina kata zifuatazo;
Vwawa,Hasanga,Ilolo,Ichenjezya,Ihanda,Isandula,Ipunga,Nyimbili;Hezya,Idiwili,Iyula,Nanyala,Ruanda na Mlangali.
Katika baraza la madiwani hilo pia yalitolewa Mapendendekezo ya kuomba kama jimbo la Igamba litakubalika basi lipewe hadhi ya wilaya.
Mgawanyo huu una kuja mhula mmoja tangu Jimbo la Mbozi magharibi lilipo pewa hadhi ya wilaya ya Momba.
Asante ya Taarifa Mdau mwenza MJUMBE BLOG,Mbozi,Mbeya.
Post a Comment