Unknown Unknown Author
Title: TUSIMPIGIE KURA MGOMBEA MASIKINI!! SABABU HIZI HAPA!!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Rais wa Kenya ,Uhuru Kenyatta ni mmoja wa matajiri wakubwa wa Afrika , inasemekana Aliachiwa urithi wa ardhi kubwa sana na baba yake ambaye...

Rais wa Kenya ,Uhuru Kenyatta ni mmoja wa matajiri wakubwa wa Afrika , inasemekana Aliachiwa urithi wa ardhi kubwa sana na baba yake ambaye alikuwa rais wa kwanza wa Kenya , Mzee Jomo Kenyatta .

Toka ameingia madarakani amefanya mabadiliko mengi na kuwajibisha wengi ya karibuni zaidi ni kuwajibisha wakuu wa mashirika ya umma zaidi ya 20 kutokana na tuhuma za rushwa .

Prof Peter Mutharika ambaye ni rais wa Malawi wa sasa alitangaza mali zake alipoingia madarakani ambazo ni dola milioni 4 za kimarekani pamoja na vitega uchumi vingine alivyonavyo na hisa .

John Kerry , Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani wakati alipotakangaza kugombea urais wa Marekani alitangaza mali zake ambazo zilikuwa zaidi ya dola milioni 30 za marekani hapo ni nyumba zake , hisa zake na jinsi anavyolipa kodi .

George Bush Mkubwa na Mdogo wote walikuwa marais wa Marekani , wote ni wamiliki wa moja ya kampuni kubwa kuliko zote za mafuta na Gesi ulimwenguni utajiri wake hausemekani lakini wote waliwahi kuwa marais wa marekani .

Rais wa Sasa wa Marekani , Barak Obama alitangaza mali zake kabla ya kuukwaa urais ambazo zilifikia dola milioni 5 atakapomaliza muhula wake wa 2 atatangaza tena mali zake na mengine mengi ambayo yatakuwa wameshakaguliwa na chama cha wahasibu wa marekani pamoja na taasisi nyingine za serikali .

Kwahiyo wewe unasema si Tajiri , lakini umekuwa waziri kwa miaka 10 , tunajua safari zako zote za nje unalipwa posho kiasi gani na msururu wa watu unaoenda nao kwa kipindi hicho cha miaka 10 , bado wewe ni mbunge unavyoenda bungeni unalipwa posho .

Ukiacha hili la uwaziri tunajua ulikuwa unafanya shuguli nyingine kama ni za serikali au binafsi kabla hujawa mbunge wala waziri huku kote ulikuwa unatengeneza maisha yako na ya familia yako na kama una mke hata mkeo nae ni mfanyakazi kwahiyo kipato chenu kwa pamoja kilikuwa kikubwa kiasi Fulani iweje leo utuambie wewe ni maskini ?

Hapa Kwetu inaonyesha mtu kuwa na hela au kuwa tajiri basi huyo hatakiwi kugombea urais au ubunge tunataka wale maskini wanaojionyesha kwamba wana hela chache na milolongo mengine mingi sana .

Kuna baadhi ya wagombea wanajinasibu masikini saa hizi lakini hawako radhi kuonyesha mapato na matumizi yao toka wameingia serikalini kwenye ngazi ya ubunge na uwaziri kwa kipindi chote .

Nikiambiwa nipige kura kati ya mgombea tajiri na maskini nitampa tajiri ambaye ameweka utajiri wake hadharani na ambao umekaguliwa na vyombo kama TRA na vingine nchini kuthibitika kwamba hazina utata wowote .

Kiongozi tajiri anatupa funzo moja kuu kwamba yeye ameongoza kampuni yake kwa mafanikio kwa kipindi Fulani kabla ya kuamua kugombea urais , anajua mambo ya mikataba , makubaliano , mikopo na masuala mengi yanayohusu biashara na maisha kwa ujumla kuliko baadhi ya wagombea .

Nchi yetu inaingia kwenye kipindi cha Uzalishaji wa Gesi , mafuta , Urani na maliasili nyingine nyingi hii inahitaji mtu mwenye uwezo huo wa biashara , maelewano , mikataba , mikopo na maendeleo si mtu yoyote tu .

Lengo la makala hii sio kumpigia kampeni Fulani , ni kusema ukweli uliopo tu ili tuweze kuwa huru .

YONA FARES MARO
0786 806028

Mtembea bure wa MJUMBE BLOG ame kaririwa akisema:
....Kujinasibu kuchaguliwa kwa misingi ya kimasikini;ni kufirisika kimawazo!

Kiongozi lazima awe mfano.Lazima aondokane na utegemezi kiuchumi.Hatuwezi kusimama imara kwa kufiria tuta simama kihohehahe.

Tuna tamani nchi yetu isogezwe kutoka hapa tulipo ili kufikia mbele!

Kumchagua kiongozi MASIKINI ni kuuchagua UMASKINI pia! Nitakuwa Mtanzania wa mwisho kuuchagua UMASIKINI.

Mfalme Suleimani hajawaji tafsiriwa kama Maskini kwenye hadithi za vitabu vitakatifu....
Aliomba HEKIMA na hakuomba UMASIKINI!

Ni miongoni mwa watawala walio wahi kuwa Matajiri kwenye vitabu vitakatifu.

Hata Mwenyezi MUNGU pia hapendi watu wake watopee kwenye umasikini,badala yake anatamani wajinasue!
Ili wawe msaada kwa wahitaji kama vile Wagonjwa,Wajane,Yatima na wazee!!

UTAWEZAJE KUWA SAIDIA WAHITAJI ile khali hata wewe ni MASIKINI??

Mwisho;tafsiri ya maisha yako ni UONGOZI tosha;Una taka UINGOZE Tanzania kuelekea kwenye Umasikini??

TUACHE USANII!!
Pia tusi wachague Wanafiki wanao utumia UMASIKINI wa tulio wengi kama daraja lao.
LAZIMA TUU CHUKIE UMASIKINI...
Lazima tusiupitishe umasikini ukae kwenye kiti cha nchi yetu.

Piga vita MAWAZO YA KIMASIKINI;
Piga vita wagombea Masikini.

ZINGATIO:
Maoni hayo hapo juu ni maoni ya mtu Binafsi.
Haya wakurishi Itikadi wala chama chochote kile wala jumuiya iwayo yote ile.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top