Unknown Unknown Author
Title: UNAPO FIKIRIA KUITEMBELEA ZANZIBAR:JIFUNZE HISTORIA YAKE KWANZA KWA KINA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Picha Na Pira Harji Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayojitawala katika mambo yake ya ndani. En...

Picha Na Pira Harji

Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayojitawala katika mambo yake ya ndani. Eneo lake ni sawa na funguvisiwa ya Zanzibar iliyopo mbele ya mwambao wa Afrika ya Mashariki karibu na Tanganyikaau Tanzania bara. Inajumuisha visiwa vikubwa vya Unguja naPemba pamoja na visiwa vidogovidogo.

Kwa jumla mikoa mitano ya Tanzania imo ndani ya Zanzibar ikiwa mitatu iko Unguja na miwili Pemba. Hadi mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 sehemu hizi zilijulikana kama Usultani wa Zanzibar.

Zanzibar inatawaliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). Raisi Amani Abeid Karume aliyekuwa mgombea wa CCM amechaguliwa mara ya pili na wananchi wote tar. 30.10. 2005 katika kura iliyopingwa na chama cha Upinzani CUF.

Zanzibar ina Bunge lake lenye wabunge 50 wanaochaguliwa kwa muda wa miaka mitano.
Mji mkuu na makao makuu ya serikali ni Jiji la Zanzibar ambalo liko kisiwa cha Unguja. Mji mkuu wa kisiwa cha Pemba ni Chake Chake. Idadi ya wakazi wote ilikuwa 984,625 mwaka 2002, wakiwa 622.459 wakazi wa Unguja na 362.168 wakazi wa Pemba.

Biashara ya Zanzibar ni kilimo na utalii. Mazao yanayouzwa nje ni hasa karafuu, basibasi, mdalasini na pilipili.
Jamhuri ya watu wa Zanzibar ilianzishwa baada ya mapinduzi ya 1964 iliyomaliza Usultani wa Zanzibar. Rais wa kwanza alikuwa Abeid Amani Karume hadi 1972 aliyefuatwa na Aboud Jumbe (1972-1984). Rais wa tatu aliyemfuata alikuwa Ali Hassan Mwinyi (1984-1995) aliyeendelea kuwa pia rais wa Tanzania tangu 1985.
Rais wa sasa ni Amani Abeid Karume ambaye ni mwana wa rais wa kwanza.
Historia
Historia inajionesha ya kwamba kiasi cha miaka 20,000 kumekuwepo makazi ya bidadamu katika visiwa vya Zanzibar. Visiwa hivi ni sehemu ya kumbukumbu ya kihistoria ya ulimwengu wakati waajemi wafanyabiashara waliigundua na kufanya ndio makao makuu kwa safari kati ya Mashariki ya Kati, India, Na Afrika.
Katika karne ya mwanzo AD Zanzibar pamoja na mwambao wa Afrika ya Mashariki ulikua katika ufalme wa Saba,Katika kipindi cha karne ya 3 na 4AD,Wabantu walianza biashara na Waarabu waliokuja Afrika ya Mashariki. Katika karne ya 7 AD,waarabu walikuja Zanzibar kibiashara pia kusambaza Dini ya Kiislam,Waarabu ndio waliyoipa jina ZANZIBAR kutokana na neno la Kiarabu ZINJI BAR yaani sehemu ya watu weusi.
Lugha ya kiswahili imeanza kutumika kiasi cha karne ya 13 AD,Lugha ya kiswahili ilitokana na kuchanganyika lugha ya kiarabu na lugha za kiafrika.
Karne ya 16 AD wareno walikuja Zanzibar lakini utawala wao ulifuatiwa na kutokuwepo utulivu,lakini biashara ya Utumwa iliwaweka watu pamoja. Waarabu kutoka Oman walichukua utawala Zanzibar katika karne ya 17 AD,Na Zanzibar ilikua ni makao makuu ya utawala wa Waomani.

1820-1870 Zanzibar ilifaidi matunda mazuri ya kiuchumi na maendeleo yaliyosababishwa na utawala wa kisultani na hivyo kupelekea Zanzibar kuwa na mwakilishi nchini marekani na kupelekea kuenea kwa Dini ya wa kiislam. Katika karne ya 19 AD Zanzibar ilikua chini ya utawala wa Oman,mwaka 1830 Zanzibar ilikua inaongoza kwa kilimo cha karafuu ,na hiyo kupelekea mahitaji ya watumwa kuongezeka kutumika katika kilimo. 1885 kamisheni kutoka Uengereza na Ujerumani iliamua kuigawa Zanzibar kutoka katika utawala wa Kisultani na ndio ulikua mwisho wa utawala wa kujitegemea kwa Zanzibar na mnamo mwaka 1886 sultani alikubali maridhiano hayo.

1890 Zanzibar ilikua chini ya uangalizi wa waingereza rasmi lakini uchaguzi wa mwanzo ulifanyika mwaka 1957,na miaka iliyofuata kukakuwepo fujo na machafuko kutoka kwa waafrika wanaodai uhuru dhidi ya utawala wa kiarabu. Mwezi wa 12 mwaka 1963 Waingereza waliipa uhuru Zanzibar chini ya jumuiya ya madola,na mwezi wa mwaka 1964 Zanzibar ilifanya mapinduzi kujikomboa kutoka katika utawala wa kisultani,muda mchache baadae iliungana na Tanganyika kuunda Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA.
Uchumi
Uchumi wa Zanzibar ni uchumi wa hali ya chini kabisa ambao mwananchi wa kawaida anaishi chini ya dola moja kwa siku au kutokua na uhakika wa kupata chochote. Hilo linatokana na viongozi wa vyama kutoonesha mori katika kutatua matatizo au kuweka mbinu za kuleta maendeleo,badala yake ni kujadili siasa kwa muda mwingi. Zanzibar ni nchi yenye matumaini katika uchumi lakini kutokana na migogoro ya kisiasa imekua katika hali duni kabisa,ni hivi majuzi tu balozi wa Marekani alisisitiza kuwa umuhimu wa kuwepo mashirikiano katika siasa ili kuiwezesha Zanzibar kuinuka katika hali ya kiuchumi.
Idadi ya Watu
dadi ya Watu na Makazi.
Watu wa Zanzibar ni wa asili mbalimbali, hasa watu wa asili ya Afrika Bantu[17]; Waasia, awali kutoka India na nchi za Kiarabu. Idadi ya wakazi wa Zanzibar ilikuwa 984,625 mwaka 2002,[18] tarehe ya sensa ya mwisho, kwa kiwango cha ukuaji wa 3.1%, . Hii, karibu theluthi mbili ya watu - 622,459 - wanaishi Kisiwa cha Zanzibar(Unguja), Mkoa wa mjini magharibi ndio wenye idadi kubwa ya wakaazi kiasi cha watu 205,870.
Pemba ina jumla ya makazi sawa. Mji mkubwa ni Chake Chake, na idadi ya 19,283, mengine ni Wete na Mkoani. Kuna tofauti kubwa katika kiwango cha maisha kati ya wakazi wa Pemba na Unguja na kati ya wakazi wa mijini na vijijini. Wastani wa mapato ya kila mwaka ya US $ 250 na ukweli kwamba karibu nusu ya maisha ya wakazi wanaishi chini ya mstari wa umaskini. Huduma ya afya vifo vya watoto wachanga bado ni 83 katika Waliozaliwa 1000 , na inakadiriwa kuwa utapiamlo huathiri moja katika tatu ya watu wa visiwa ', matarajio ya maisha wakati wa kuzaliwa ni 48. Wakati matukio ya VVU / UKIMWI ni ndogo mno kwa Zanzibar kuliko Tanzania kwa ujumla (0.6% ya idadi ya watu, kama dhidi ya wastani wa kitaifa wa%8).
Dini
Dini ya Uislamu ni kiasi cha 97% . Mchanganyiko iliyobaki ni mchanganyiko wa Hindu na wa kikristo.
Dini za kihindi pia zipo katika visiwa hivyo, lakini wengi wao walikimbilia nchi au kuuawa wakati wa mapinduzi ya 1963. Wakristo walikuja baadaye wakati wa kipindi cha utawala wa Kireno na ukoloni wa Uingereza.

Kuna misikiti 51, ambaye waadhini hugongana kwa kila mmoja wakati wa maombi, pamoja na Majumba ya Hindu sita mahekalu na Kanisa Kuu Katoliki kama vile Kanisa Kuu Anglican katika mji wa Zanzibar Stonetown).


Usultani wa Zanzibar

Usultani wa Zanzibar ilikuwa nchi kwenye pwani la mashariki ya Afrika kati ya 1856 na 1964. Tangu 1890ilikuwa nchi lindwa chini ya Uingereza.


Ilianzishwa wakati wa kugawa Usultani wa Omani mwaka 1856 ikaishia mwaka 1964 baada ya mapinduzi ya Zanzibar na muungano na Tanganyika.
Sayyi Said kuhamia Unguja
Usultani ulianzishwa wakati Sultani Sayyid Said alipoamua kuhamisha makao makuu yake kutoka Maskat(Omani) kwenda Unguja. Sayyid Said alikuwa Sultani wa Omani tangu 1804. Aliimarisha utawala wa Omani juu ya pwani la Afrika ya Mashariki. Mwaka 1829 alifaulu kuteka Mombasa iliyokuwa mji wa pekee wa kujitegemea kati ya miji yote ya Uswahilini.
Visiwa vya Unguja na Pemba vilikuwa chini ya Omani tangu 1689 Wareno walipofukuzwa katika pwani za Uswahilini.
Biashara ya karafuu na watumwa
Sayyid Said aliona nafasi kubwa ya biashara ya karafuu kwa ajili ya soko ya Uhindi na penginepo. 1829 akaanzisha mashamba ya mikarafuu kwa kutumia kazi ya watumwa kutoka bara. Biashara ikabadilisha uso wa mji wa Zanzibar ya karne ya 19 iliyowahi kuwa kijiji kikubwa tu ya vibanda kando la boma lililojengwa na Omani kama kizuizi dhidi ya Wareno.
Baada ya azimio la mwaka 1832 la kuhamisha mji mkuu wa Omani kwenda Unguja idadi ya wakazi wa mji ulikua haraka. Nchi za nje zikatambua mji mkuu mpya na kujenga uhusiano. Ubalozi wa Marekani ulijengwa 1837, Uingereza ukafuata 1841 na Ufaransa 1844. Sultani mwenyewe aliondoka Maskat kabisa mwaka 1840. Kukua kwa Zanzibar kulisababisha kukonda kwa mji wa Maskat
Baada ya kifo cha Sayyid Sultan mwaka 1856 usultani wa Oman uligawiwa kati ya wanawe. Sayyid Majid bin Said Al-Busaid (1834/5–1870) akawa Sultani wa kwanza wa Zanzibar na kakaye Sayyid Thuwaini bin Said al-Said akawa Sultani wa Oman akitawala nchi bila maeneo ya Afrika ya Mashariki.
Kugawiwa kwa Omani ilikuwa mwanzo wa Zanzibar
Usultani mpya ulikuwa nchi yenye nguvu kati ya Rasi Delgado (mpakanani na koloni ya Kireno ya Msumbiji) hadi Mogadishu. Athira yake ilienea kupitia njia za misafara ya pembe za ndovu na watumwa hadi mto Kongo. Wafanyabiashara kama Tippu Tip waliokuwa raia wa Usultani wakapita Tabora na Ujiji kwenda ziwa Tanganyika na kuingia ndani ya Kongo. Wapagazi wao walibeba bidhaa kutoka Zanzibar zilizobadilishwa kwa pembe za ndovu hasa. Watumwa walikamatwa au kununuliwa wakabeba pembe hadi pwani.
Sultani wa pili wa Zanzibar penyewe Sayyid Bargash alijitahidi kujenga uhusiano na nchi za nje. Alifunga soko la watumwa Zanzibar mjini kulingana na mapatano ya mimataifa lakini akavumilia biashara ya watumwa kuendelea chinichini. Wakati wa Bargash majengo mengi ya Mji Mkongwe yakajengwa.
Sayyid Bargash
Mwishowe wa utawala wake aliona kupungukiwa wa eneo lake kutokana na mashindano ya nchi za Ulaya ya kuenea katika Afrika baada ya mkutano wa Berlin. 1885 Karl Peters alifanya mikataba ya ulinzi na watawala wadogo barani ya Tanganyika waliokuwa chini ya Sultani. Upingamizi wa Sultani ulishindikana kwa sababu Wajerumani walitumamanowari Unguja akapaswa kukubali maeneneo mapya ya Wajerumani.
Kuenea kwa ukoloni

1886 mkataba kati ya Uingereza na Ujerumani ulibana eneo la sultani barani katika kanda yenye upana wa maili kumi kati ya Rasi Delgado na Mogadishu. Bargash na mfuasi wake Khalifa bin Said waliamua kuuza maeneo haya au kuyakodisha.
1887/8 pwani la Kenya ikakodishwa kwa Waingereza. Wakati wa uhuru wa Kenya sehemu hii ikaingizwa katika Jamhuri ya Kenya.
Pwani la Tanganyika ikakodishwa kwa Wajerumani mwaka 1888 na kuuzwa mwaka 1890.
Miji kwenye pwani la Somalia ikakodishwa kwa Italia mwaka 1892 ikauzwa 1906, Mogadishu 1924.
Hali halisi usultani ukabaki na visiwa viwili vya Unguja na Pemba tu.
Waingereza walikuwa walisita kuhusu Zanzibar lakini baada ya jaribio la Karl Peters la kufanya mkataba wa Sultani na kuingiza visiwa katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani Uingereza uliamua kutafuta utawala wa visiwa.
Mkataba wa Zanzibar-Heligoland na mwisho wa uhuru
Mkataba wa Zanzibar-Helgoland kati ya Ujerumani na Uingereza ulileta patano la kuwa Zanzibar itakuwa chini ya Uingereza. Tangu 1890 waziri mkuu wa Sultani alikuwa Mwingereza aliyeopkea amri zake kutoka London. Tangu 1913 nafasi ilichukuliwa na afisa mkazi mkuu.
Kwa muda wa miaka 26 usultani ulikuwa na fedha yake ya pekee iliyoitwa Riali ya Zanzibar.
Uhuru 1963 na mapinduzi
Zanzibar ilipata uhuru wake 10 Desemba 1963. Uhuru wa usultani ukadumu muda kidogo tu. Mapinduzi ya 12 Januari 1964 yakampindua Sultani. Mauaji ya familia nyingi zenye asili ya kiarabu yakafuata. 26 Aprili 1964 Zanzibar ikaunganika na Tanganyika kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Masultani wa Zanzibar
Sayyid Said (1856–1870)
Barghash bin Said (1870–1888)
Khalifah bin Said (1888–1890)
Ali bin Said (1890–1893)
Hamad bin Thuwaini (1893–1896)
Khalid bin Barghash (1896)
Hamud bin Muhammed (1896–1902)
Ali bin Hamud (1902–1911) (abdicated)
Khalifa bin Harub (1911–1960)
Abdullah bin Khalifa (1960–1963)
Jamshid bin Abdullah (1963–1964)
Mawaziri
Sir Lloyd William Matthews, (1890 hadi 1901)
A.S. Rogers, (1901 hadi 1906)
Arthue Raikes, (1906 hadi 1908)
Francis Barton, (1906 hadi 1913)
Maafisa wakazi wakuu
Francis Pearce, (1913 hadi 1922)
John Sinclair, (1922 hadi 1923)
Alfred Hollis, (1923 hadi 1929)
Richard Rankine, (1929 hadi 1937)
John Hall, (1937 hadi 1940)
Henry Pilling, (1940 hadi 1946)
Vincent Glenday, 1946 hadi 1951)
John Sinclair, (1952 hadi 1954)
Henry Potter, (1954 hadi 1959)
Arthur Mooring, (1959 hadi 1963)



MJUMBE BLOG Tuta kuletea Mfululizo wa vitutio vya Kitalii Zanzibar;hivi karibuni endelea kututembelea mtandaoni.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top