Unknown Unknown Author
Title: YEYE ATIA NIA:WAHAFIDHINI WA LOWASA WAMCHAMBUA KUANZIA UNYAYONI MPAKA UTOSINI!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
UCHAMBUZI  KUTOKA  KWA  Malisa Godlisten 1. Asilimia zaidi ya 90% ya watu waliokuwepo uwanjani wamegharamiwa. Bodaboda walilipwa, Wanafunz...

UCHAMBUZI  KUTOKA  KWA  Malisa Godlisten
1. Asilimia zaidi ya 90% ya watu waliokuwepo uwanjani wamegharamiwa. Bodaboda walilipwa, Wanafunzi walisafirishwa, Waandishi walilipwa. Wachache walioenda kwa hiari yao walienda kushangaa tu wala sio mashabiki wa Lowassa. This is to say ikiwa Lowassa asingetumia pesa huenda uwanjani angekua yeye na familia yake tu.
2. Wengi wanaomuunga mkono Lowassa ni "opportunists". Ni watu wanaotegemea akiingia madarakani awakumbuke. Either awape vyeo au awape unafuu kwenye biashara zao. Hakuna yeyote kwny kundi la Lowassa anayemuunga mkono kwa lengo la kuisaidia nchi.
3. Afya ya Eddo imedhoofu sn na hawezi kuwa Rais wa nchi. Alipoingia uwanjani ameshindwa kupanda ngazi za jukwaa, akasimama katikati ya ngazi kwa dakika chache kabla ya kusaidiwa kupanda. Pia anaongea kwa Shida, na mikono yake haina nguvu. Hali hii imesababisha ashindwe kushika microphone alipopewa "mike" na Kibonde. Mzee Kingunge yupo fit kiafya kuliko Eddo.!
4. Mkutano wa Lowassa leo ni biashara kama zilivyo biashara nyingine. Kuna watu wamepata hela ya kulipa mahari kupitia mkutano huu, kuna waliopata mitaji ya kukuza biashara zao na kuna waliopata lift za bure za kwenda Arusha kufanya mambo yao. Hii inaitwa "mbwa kala mbwa"
5. Kutokana na maelezo ya Eddo ni wazi kuwa ana "bifu" na JK. Amekiri kuwa alimpigania sn Kikwete 1995 na 2005 lakini inavyoonekana JK amemsaliti.
6. Akiingia madarakani atalipiza kisasi kwa wabaya wake wote hasa Samuel Sitta, Anthony Diallo na vibaraka wao wote. Ikiwa Eddo atashinda kuna dalili Sitta, Dialo, Makonda, na vibaraka wengine wa CCM wakaishia jela.!
7. Mkutano wa leo ulikua ni mkwara wa kuionesha Kamati kuu ya chama chake kuwa ana nguvu kiasi gani, ili wasijaribu kabisa kukata jina lake wakihofia kukipasua chama.
8. Safari ya matumaini ni safari ya matamanio. Au unaweza kuiita safari ya matumizi. Huwezi kutumia 1.4 bilion for just a single day wakati kuna watu wanakufa kwa kukosa "padadol" ya shilingi mia halafu ukasema ni matumaini. Labda matumaini ya kuuza nchi.!
9. Ikiwa Eddo atashinda Yuko tayari kutumia rasilimali za nchi ili kulipa fadhila kwa rafiki zake waliomuunga mkono wakati wa kugombea. Kwa mfano yupo tayari kumgawia Mengi vitalu vya gesi Mtwara na kuwaacha watanzania wasinufaike na gesi yao kisa tu Mengi alimpa support kwny kugombea.
10. Lowassa ni msanii mzuri wa sanaa za maonesho. Ametumia makundi yote mawili ktk kufanikisha azma yake. Kundi la Maskini na kundi la matajiri.Ametumia maskini kwa kuwaahidi kuwa atawabana matajiri walipe kodi ili kuboresha maisha ya maskini.
Na ametumia matajiri akiwaahidi kuwa atawabana maskini ili wasipige kelele wakati anawagawia matajiri rasilimali za nchi. Hii ni sanaa. Ha hakika hapa Eddo ameitumia vizuri elimu yake ya sanaa ya chuo kikuu cha Dar es Salaa. (B.A in Fine &Perfoming Arts).!
NB: Watanzania hawawezi kuruhusu kumpa nchi hii "msanii". Nchi hii inatakiwa kuongozwa na mtu "real". Na mtu real hawezi kupatikana kwingine nje ya UKAWA.!
‪#‎SAY_NO_TO_SANAA‬
‪#‎SAY_NO_TO_CCM‬
‪#‎BE_REAL‬. ‪#‎VOTE_FOR_UKAWA‬.


Beni wa

Mtu anataka kuwa Rais kupitia CCM lakini ana-copy na ku-Paste ilani ya CHADEMA 2010 na sehemu kubwa ya Ilani ya chama cha ACT ya Sasa
Halafu anaongezea ujinga mwingi kama wa kumaliza Foleni kwa miezi 12 tu
Hivi kuhusu kuondoa umasikini ameonyesha Economic analysisi yoyote? Ata-harmonize vipi mageuzi ya Kilimo na Viwanda na Kutengeneza Middle Class kama anavyonukuu Malysia na mataifa mengine.
Comedian at work!
Angalao hajafanya ule ujinga wa kutukana watu kama alivyofanya last week.
Ile shahada yake ya Kwanza (B.A Theatre) ameikumbuka tena leo
Hupendi umasikini lakini unawaibia masikini na kuwasifu maswahiba wako wanaoibia Masikini.Miaka yote hakuyaona haya ?
Yaani huko CCM hakuishi vituko.
Aluta Continua,Victory Ascerta...
Ben Saanane



Kufuatia tukio la leo la Kile kiliichoitwa kuzinduliwa kwa safari ya matumaini; Nina Haya ya kusema..
1: pesa inaweza kununua Kila Kitu na kuubadili Uongo kuwa ukweli..
Inaweza kumbadili fisadi aonekane msafi; mwenye macho awe kipofu; Mwenye masikio awe kiziwi lkn kubwa Zaidi; Mwenye utambuzi awe km mwendawazimu..
Inashangaza umati ule unaleta picha gani?
Nilishtuka kuwaona watu km Akina Mzee kingunge ambao wanajua kabisa lowassa ni nani..
2: Vijana wengi Wa taifa hili ni Vijana wasiojua nchi kwa Sasa inahitaji nn..
Ni Tanzania tu ambapo Vijana wanaweza kumshabikia fisadi aliyewahi kuwajibishwa na bunge..
Ni Tanzania tu ambapo kijana asiye na ajira anaweza kumshangilia waziri (na pia kawa pm) ambae katumikia taifa kwa miaka 38 na hakupata dawa ya tatizo la ajira.
3: lowassa ni mgonjwa..
Ukiangalia anavyotembea; kuongea na kucheza; utagundua hiki Kitu.
Hata kauli yake Eti wagombea wapimwe ni defensive mechanism tu..
4: tatizo la msingi la nchi yetu halijui..
Tatizo kubwa la nchi hii kwa Sasa ni vita dhidi ya ufisadi..
Lowassa hajalipa hili uzito Mkubwa kwenye maelezo yake..
Nadhani saga ya Richmond inamuumiza..
Ukiisoma hotuba yake (kwa waliosikiliza pia ni mashahidi); ufisadi hajalipa kipaumbele sana na hajatoa tiba ya tatizo hilo Sugu linalotafuna taifa kwa ss..
5: nchi imeyumba...
Lowassa kadhihirisha hili kwa maneno..
Km nchi imeyumba na liwassa katumikia taifa hili km kiongozi mwandamizi kwa miaka 38; ni dhahiri yeye ni sehem ya kuyumba kwa taifa hili kiuchumi na kijamii..
Akili ile ile iliyoshiriki kuyumbisha nchi Eti leo inataka kutuaminisha inataka kutatua matatizo yetu..
Hiki ni kichekesho..
6: nimuunge mkono kuwa; nchi hii inahitaji kiongozi anayeweza kuchukua hatua kwa wakati; kiongozi anayechukia umaskini; atakayebuni mikakati ya ajira kwa Vijana na atakayeweza kuboresha elim na kuigeuxa nchi hii kuwa nchi isiyotegemea misaada..
Mtu Huyo; hatatoka CCM..
Mwisho; niwaombe wapenda mabadiliko wasitishwe na maigizo Yale ya siasa kwa nguvu ya pesa za Richmond ambazo aliahidi atatolea ufafanuzi lkn akakacha baada ya mkwara Wa mwakyembe..
Tusonge mbele..
Vita imeanza...
Ally Rama (masomoni SEKOMu)
0656294262




Hivi mnawezaje kukaa na kufuatilia maigizo na kuamini asemacho? Lowasa alisoma BA Fine and Performing Arts, ni mwanamazingaombwe msomi.
Viongozi wa dini aina ya Gwajima ni mabakuli ya wanasiasa, pesa yako tu utaamua aseme nini. Wiki iliyopita alikuwa alisema ameotesha na Mungu wake kuwa Slaa ndie Rais mpya ajae, Leo tena amesema ameonyeshwa na Mungu wake kuwa Lowasa ndie Joshua wa kwenye biblia aliyewavusha Israel. Hivyo atawavusha wa Tanzania ikiwa atakuwa Rais


UCHAMBUZI  KUTOKA  KWA   Yericko Nyerere

Hawa walisherekea kifo cha Mwalimu Nyerere, leo wanamtumia kuutaka urais!
Yericko Nyerere 23:26 Today
Tuachane na Josephat Gwajima anayejiita ni mchungaji japo sijui nani alimtunuku uchungaji na kwavigezo vipi, yeye hana tofauti na sigara kali
Aliyekuwa anaamini Kingunge ni kiongozi wa kitaifa atafakari upya,Jiulizeni kwa nini hakupata nafasi ya juu kama Mzee Kawawa enzi ya mwalimu?
Ni Kingunge huyuhuyu alifukuzwa ukuu wa mkoa singida na Mwalimu Nyerere, leo anajivika chanda cha Mwalimu.
Lowa alifukuzwa uanachama wa TANU kwakosa la kuiba pesa ya ujenzi wa ofisi za umoja wa vijana wa Tanu jijini Arusha yeye akiwa ni katibu wa vijana mkoa,
Ni Moringe na baadhi ya wazee waliopiga magoti kumuombea punguzo la adhabu na hivyo akapewa adhabu ya kuwepo Lumumba tu bila kazi yoyote kwa mda wa mwaka mzima.
Katibu wa vijana TANU Taifa ndugu Elly Anangisye alifukuzwa moja kwa moja na ubunge wa Rungwe akavuliwa.
Alipofariki tu Mzee Nyeree, Lowasa na kundi lake walifanya party na kupongezana, wengine walipigiana simu hata kabla hajafa kuwa kikwazo kimeondoka,
Leo kutangaza nia ya urais wanamtaja Mwalimu kama mbeleko.
Rip J.K Nyerere

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top