Wakazi wa Ubungo wakiwa kwenye foleni ya
kujiandikisha vitambulisho vya kupiga kura kwa
mfumo wa BVR
BVR Dar, rushwa nje nje!
Na: Sarafina Lidwino;
IKIWA ni siku ya tatu leo, tangu zoezi la la
uandikishaji wa Daftari la upigaji kura kutumia
mfumo mpya wa Kielektroniki (BVR) kuingia Jijini
Dar es Salaam rushwa imeonyesha kutawala
kwa baadhi ya vituo vya uandikishaji . Anaandika
Sarafina Lidwino … (endelea).
Licha ya kuanza kwa zengwe tangu siku ya
kwanza zoezi hili lilipoanza, kutokana na
matatizo mengi kujitokeza katika vituo rushwa
imewakosesha wananchi wengi haki zao za
msingi.
Changamoto nyingine ambazo
zilikuwa zimejitokeza sana
kwa siku za kwanza zilikuwa
ni pamoja na, ubovu wa
mashine, kuchelewa kwa
waandikishaji vituoni hapo
pamoja na kutowapa
kipaumbele makundi maalum.
Kutokana na matatizo hayo na mengine mengi,
Gazeti la MwanaHalisi Online lilifunga safari na
kutembelea baadhi ya vituo vya Wilaya ya
Kinondoni na Ilala, na kuweza kubaini matatizo
mengi likiwemo la rushwa.
Moja katia ya vituo vichache kati ya vingi
ambavyo ambavyo vilitembelewa ni pamoja na
kituo cha Kinondoni Biafra, Mkwajuni, Ilala
Bungoni, Buguruni ambapo lilibainika tatizo
kubwa la rushwa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kati ya
wahanga hao ambao wamepoteza haki zao za
msingi kutokana na kutokuwa na pesa za
kuhonga, wameilalamikiwa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC), na kusema haikujipanga kwa
zoezi hilo.
Akielezea mmoja kati yako, Mkazi wa Ilala
Bungoni (hakutaka kutaja jina) ameelezea
kuhusu rushwa inavyotendeka kituoni hapo na
kusema, “kunawatu wenye pesa zao ambao
wanakuja hapa hawakai foleni bali wanatoa tu
pesa”
Amesema, “tukiwa kwenye foleni utashangaa tu
mtu anaenda kule mbele anatoa hela kisha
anapewa namba kwa hiyo wanawauzia namba
za mbele ili kesho yake wapate kitambulisho
mapema”.
Amesema, hali hiyo imekuwa kero kwa wananchi
wa hali ya chini, ambapo muda mwingine
hupelekea kutokea kwa fujo vituoni kutokana
kwamba inakuwa ngumu kuona mtu akitumia
mabavu kupata haki.
Naye mkazi wa Mkwajuni, Rebeka Salum
ambaye alikuwa katika foleni ya kujiandikisha,
alisema,
“mbali na hilo la rushwa lakini pia lipo
la kero ya matusi na lugha mbaya kutoka kwa
hudumu wa vituo vingi.
Salumu amesema, inaonekana baadhi ya
mawakala wengi hawakupatiwa elimui ya
kutosha kuhusu uandikishaji kitu ambacho
kinwapelekea mawakala wengi kugombana na
waandikishwaji.
Akizungumzia tatizo la rushwa na lugha chafu
zinazotolewa na mawakala hao leo Mkuu wa
mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq
amewataka wananchi wanaokubwa na matatizo
hayo kutoa taarifa mapema sehemu husika.
Sadiq amesema, anashangwazwa sana na
vitendo vinavyofanywa na mawakala hao kwani
kabla ya kuanza kwa zoezi hili walipewa
mafunzo ya kutosha.
“Mimi binafsi pia nimeshapata meseji nyingi
kutoka kwa wananchi tofauti wakilalamikia
matatizo haya, japo jana nilijaribu kutembelea
katika baadhi ya vituo vya hapa Dar na sikuliona
hilo tatizo la rushwa”.amesema.
Aidha,metoa wito kwa wananchi ambao
wanakutwa na matatizo hao watoe taarifa kwa
viongozi husika na wasikubali kutoa rushwa
wanazodaiwa bali wawakamate na kuwafikisha
sehemu husika.
Chanzo:Mwanharisi Online
Post a Comment