
Pichani ni Mzazi aliye jitambulisha kama Ndugu Daniel Mtweve(mwenye kofia nyekundu) na kijana wake Paul D Mtweve.
Asubuhi ya leo Kamera yetu ya MJUMBE BLOG ime jikuta ikivuta usikivu kwenye mzungumzo kati ya mzazi na kijana wake....
Yaliyo fanyika kando ya ubao wa matokeo.
Ambapo mzazi huyo aliye kuwa katoka safari ya zaidi ya Km 60 na mahitaji ya mwanaye huyo ali omba aoneshwe matokeo ya mwanae huyo ambaye katika alama zake alikuwa ame pata daraja la 'MERIT'.
Paul D Mtweve ni nani?
Ni miongoni mwa watahiniwa walio fanya vizuri darasani mwake kwenye mitihani ya MOCK kidato cha nne katika shule ya Sekondari Mundindi iliyopo kata ya Mundindi,Liganga;Ludewa.
NINI KILICHO MVUTIA MPIGA PICHA wetu?
Huku aki sogea ubaoni hapo yalipo bandikwa matoeo hayo alishuhudia hakuna mwanafunzi aliye pata alama ya MERIT mwingine zaidi ya kijana huyo!
ILIKUWAJE BASI:
Katika alama zote alizo pata kijana huyo kulikuwepo alama ya F Moja na D Moja tu Lakini mzazi huyo ali endelea kumsihi na kumuhoji kijana wake huyo kuwa HIZI ALAMA KWENYE MASOMO HAYA UME ZITOA WAPI?
Kwanini upate F na D?
....Kijana akiwa ame tahamaki na kukaa kimya; huku aki yaonea haya matokeo hayo!
Mzazi kwa lugha ya ukali na ujasiri '...yaani sisi tuna toa mahitaji huku halafu wewe una pata F na D?
Naomba muda ulio bakia hakikisha una ondoa hizi alama za F na D...
Haijalishi wengine wote watafeli au wame pataje alama!
Jitazame wewe ume pataje?
Usianze kujilinganisha na wengine wala kufurahia matokeo yako ya jumla wakati una alama kama hizi za F na D!
....KIPI KILICHO GEUKA KIVUTIO?
Paul D Mtweve ndiye aliye pata alama za juu zaidi katika darasa lake lenye wanafunzi jumla ya 60!
Akipata alama zingine zote kwenye daraja la B na +B ukiondoa masomo mawili hayo aliyo pata F na D saba ame fanya vizuri mno.
Pamoja na kuonekana ndiye aliye pata alama nzuri zaidi kwenye mitihani yao ya Mock....
Lakini mzazi ana onesha kuto ridhishwa na F na D zake kwenye masomo hayo na ame mwachia changamoto kuhakikisha ana zifuta ili abadili matokeo yake zaidi.
Mdau wa MJUMBE BLOG anapata fursa ya kuongea na baadhi ya walimu wa Paul D Mtweve;kuhusu alama hizo...
Wana kili kwamba hata wao hawaku wahi kufikiria kumgombeza mwanafunzi huyo kwa alama hizo kitendo alicho kifanya mzazi huyo kime wapa fundisho zito zaidi.
Fundisho la kuamini kuwa haijalishi ume kuwa wa ngapi darasani; alama mbili tu utakazo feli zinatosha kukufanya usutwe na kupewa onyo kali na masharti magumu ya kuzifuta pia.
Kwa maana ya kwamba alama ulizo fanya vizuri zaidi hazi futi alama utakazo fanya vibaya.
What a great lesson?
What a great insipiration?
Wakati kuna wazazi hawajui matokeo ya watoto wao wala hawa wajui wanao wana endeleaje kitaaluma na nidhamu zao kwa ujumla.
kuna wazazi wana fuatilia herufi kwa herufi na neno kwa neno kwenye matokeo ya watoto wao.
Bravo! Daniel.
Shikamoo Mtweve wa Mapogolo,Ludewa.
HITIMISHO:
Mdau wetu ana amini kuwa matokeo mazuri ya Paul D Mtweve, Hayakupatikana kwa bahati mbaya....
Haya kupatikana kwa kupewa majibu bali ni kama dedication ya kijana huyo kwa imani waliyo nayo wazazi wake kwake.
Ambayo kila akiingia kwenye mtihani huwa ana isikia sauti ya mzazi wake ikimwambia F na D sio alama zako unazo stahili wewe...
Wewe alama zako zote ni zaidi ya wastani.
Naam;
HAIJALISHI WENGINE WOTE WAME PATAJE? JITAZAME WEWE....!
Mteve Daniel;ni mfano wa kuigwa na wazazi/walezi wote ndani ya jamii.
Post a Comment