Walichosema Dr. Slaa, J. Makamba, Peter Msigwa, Kuhusu Lowassa kuhamia Chadema
BY JOSEFLY ON JULY 27, 2015 NEWS
Masaa machache yaliyopita zilisambaa picha zinazoonesha Mkutano Mkuu wa Chadema uliohudhuriwa na viongozi wote wa ngazi za juu wa chama hicho, huku aliyekuwa waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa akionekana kwenye meza kuu ya kikao hicho hali inayoashiria wazi kuwa amejiunga rasmi.
Picha hizo zisizokuwa na maelezo ya kutosha japo lugha ya picha inatoa maelezo ya jumla, zilipata maelezo mbalimbali na kuzua mjadala mrefu kwenye mitandao ya kijamii.
Baadhi ya wanasiasa wakubwa tayari wameshatoa maoni yao huhusu picha hizo na tukio zima linaloashiria kuwa Edward Lowassa amehamia rasmi katika Chama Cha Demokrasia na Maendeo (Chadema).
Naibu Waziri wa Sayansi, Mawasiliano na Teknolojia, January Makamba, kupitia tweeter ameeleza kuwa hatua hiyo imerahisha zaidi kazi ya CCM kwenye uchaguzi mkuu.
“The election just got easier for CCM,” ametweet Makamba masaa machache baada ya tukio hilo kuonekana kwenye mitandao.
The election just got easier for CCM.
— January Makamba (@JMakamba) July 27, 2015
Naye kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amepost picha hizo kwenye mitandao ya kijamii nakueleza kuwa uchaguzi wa mwaka 2015 unavutia. “It is offficial. CHADEMA central committee welcomes ex premier Edward Lowasa. 2015 very exciting elections.”
It is offficial. CHADEMA central committee welcomes ex premier Edward Lowasa. 2015 very exciting elections pic.twitter.
— Zitto Ruyagwa Kabwe (@zittokabwe) July 27, 2015
Battle lines to be drawn. Elections will easily be defined and the people will have a choice amongst LINES pic.twitter
— Zitto Ruyagwa Kabwe (@zittokabwe) July 27, 2015
Maria Sarungi, mwanaharakati ambaye ni mwanaharakati mwenye ushawishi wa kati kwenye mtandao wa Twitter na anaefahamika zaidi kwa kuendesha mijadala kwenye mtandao huo, kabla ya kuandika tweets zinazowataka watu wasubiri kusikia tamko rasmi la Chadema, alitweet:
Ego is the largest. They are ready to flout rules and principles to satisfy the Ego .. ndo kiini cha tatizo ..
— Maria Sarungi Tsehai (@MariaSTsehai) July 27, 2015
Tweet ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dr. W. Slaa iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu, ilikuja kwa mfumo tofauti na wengi waliokuwa wanaufikiria. Slaa ambaye aliwahi kuwa Padre wa Kanisa Katoliki, aliweka fumbo kwa kunukuu kifungu cha Biblia kinachoweza kukuunganisha moja kwa moja na tukio hilo.
And if a house be divided against itself, that house cannot stand. – Mark 3:25
— Dr Willibrord Slaa (@willibrordslaa) July 27, 2015
Hata hivyo, kabla picha hizo hazijasambaa kwenye mitandao ya kijamii, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa alitweet jina la ‘LOWASSA’ kwa herufi kubwa kama nilivyoandika na baadae kupost picha inayomuoesha akiwa na mbunge huyo wa Monduli, masaa matano kabla picha hizo hazijasambaa mitandaoni.
Lowasa kuondoka CCM ! pic.twitter.
Peter msigwa (@MsigwaPeter) July 27, 2015
Awali, baadhi ya wabunge wa Chadema waliwahi kueleza nia ya kumpokea Edward Lowassa katika chama chao baada ya kuwepo tetesi nyingi za mwanachama huyo wa zamani wa CCM kukihama chama hicho.
Taarifa zinaeleza kuwa Lowassa atatambulishwa rasmi kesho kama mwanachama wa Chadema na huenda akawa ndiye aliyepewa jukumu la kupeperusha bendera ya Ukawa kwenye uchaguzi mkuu akiwania nafasi ya urais.
Edward Lowassa aliondolewa katika kinyang’anyiro cha uraisi kupitia CCM, uamuzi ambao yeye na timu yake uliupinga na kudai kuwa ulifanywa kwa maslahi ya baadhi ya viongozi wa Chama hicho.
SOMA MAELEZO ZAIDI:
#Kitila Mkumbo;
In my article in The Guardian on Sunday of 28th
June 2015, among other things, I said:
"Predictably, CHADEMA is hoping to benefit from
CCM’s nomination squabbles, and it could field
one of the CCM leftover candidates for
presidency".
This attracted scathing attack from my 'friends' in
CHADEMA. I hope that they will be courageous
enough to say the three word sentence: "We are
sorry"
Ndugu Kitila, you saw it coming. Hongereni
sana kwa ujasiri watani zetu!!
and then in the same article I raised the following
questions, which can now be answered perfectly
well with great certainty:
There are clearly two big questions that will
continue to boggle the minds of political analysts
in the run up to CCM’s nomination day on the
12th July 2015. First, how can CCM avoid
nominating Lowassa in the context of his massive
following within and outside the party? Second, in
the unlikely event that Lowassa is prematurely
removed from the ballot paper in the CCM
nomination process, will he have the audacity to
join the opposition? We will have to wait for at
least two weeks until July to be able to answer
these questions.
and this was my conclusion in case Lowassa was
axed from the CCM's nomination process:
"In any case, Lowassa’s axing and eventual
joining of the opposition would be welcome by
progressive elements in the country who have
eagerly waited for decades for the splinter of the
CCM; this could surely mark the beginning of the
end of the party’s hegemony in Tanzania’s
politics".
Or will it? Let the drama begin. This is likely to
be the most charm election in the history of
Tanzania!
Kitila Mkumbo
Monday, 27 July 2015
Maelezo zaidi:
Yale yaliyokuwa yanasemwa kuwa Mbunge
wa Monduli EDWARD LOWASA atajiunga
na umoja wa katiba ya wananchi ukawa
sasa imekuwa rasmi baada ya umoja huo
kujitokeza muda huu na kumkaribisha
rasmi na kusema kuwa sasa anakaribishwa
yeye pamoja na watanzania wengine kuwa
wanakaribishwa kujiunga na harakati hizo.
Katika mkutano wa wanahabari
uliomalizika muda huu hapa makao makuu
ya chama cha wananchi CUF mkutano
ambao umehudhuriwa na wenyeviti wote
wa vyama hivyo wamesema kuwa sasa
rasmi wanamkaribisha lowasa kujiunga na
harakati zao kwani bado wanaamini ni mtu
safi ambaye alichafuliwa na watanzania
bado wanaimani nao japo kuwa alitemwa
katika mchakato wa chama cha mapinduzi.
Mh mbatia anasema kuwa umoja huo lengo
lake ni kuondoa mfumo uliopo ambao
unaongozwa na CCM hivyo wwatafanya kila
njia ambayo itasaidia kufanikisha zoezi
hilo.
Maswali mengi ya wanahabari yalikuwa
yakiwataka viongozi hao kuonyesha kuwa
LOWASA sio fisadi kama ambavyo waliwahi
kumshambulia viongozi hao wamesema
kuwa kiongozi huyo sio fisadi kwani hadi
sasa hana kesi yoyote mahakani ya ufisadi.
Kuhusu mgombea wa urais wa umoja huo
mbatia anasema kuwa mwanzoni mwa
mwezi wa nane huku mwenyekiti wa
chama cha NLD anasema kuwa hakuna
ubaya kama wakimchagua mh LOWASA
kugombea nafasi hiyo.
Mkutano umemalizika kwa viongozi hao
kusema kuwa UKAWA iko imara na ndio
tumaini jipya la watanzania na hakuna mtu
wa kuivuruga.
Post a Comment