Unknown Unknown Author
Title: SERIKALI KUKUSANYA MILION 12 KAMA MAPATO YA NDANI....!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kushoto) akisaini Mkataba wa Makubaliano ya kukusanya Sh. milioni 12,362,969 za mapato ya ndani kwa mwak...

Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kushoto) akisaini Mkataba wa Makubaliano ya kukusanya Sh. milioni 12,362,969 za mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2015/2016 hivi karibuni jijini Dar es salaam ambayo yanakusanywa kwa mara ya kwanza nchini. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bernard Mchomvu.

Na Eleuteri Mangi- MAELEZO:

Serikaki imesainiana Mkataba wa Makubaliano ya kukusanya Sh. Milioni 12,362,969 za mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2015/2016 ambayo yanakusanywa kwa mara ya kwanza nchini.

Mkataba huo wa makubaliano umesainiwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam kati ya Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bernard Mchomvu kwenye hafla iliyohudhuriwa na baadhi ya viongozi na watendaji wa Wizara ya Fedha na TRA.

 “Hakikisheni mnakusanya mapato kama ilivyopangwa na kufikia malengo tuliyojiwekea katika kukusanya mapato ya ndani katika mwaka huu wa fedha” alisema Waziri wa Saada.

Waziri huyo aliwaasa watendaji wa TRA  kuwawekea wafanya kazi mazingira mazuri ya kutekeleza wajibu wao inavyopaswa na wanapokwenda kinyume na makubaliano ya kazi watawajibishwa kwa mujibu wa sheri, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRA Bernard Mchomvu alimhakikishia Waziri wa Fedha kuwa watafikia lengo walilokubaliana kukusanya na hata kuzidi kiwango hicho ambacho kimeainishwa katika bajeti ya Serikali.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top