Walinzi wa italia wanasema kuwa takriban wahamiaji 3,000 wako mashakani
Walinzi
wa pwani wa Utaliano wanasema kuwa wanaongoza shughuli za kuwaokoa
wahamiaji kama elfu-tatu hivi ambao wametuma ishara ya kuwa taabani
kwenye mashua nje ya pwani ya Libya. Mashua kadha zinashiriki katika
uokozi.
Mashua kama 18 za raba na mashua nyengine zilizojaa wahamiaji zimetuma ujumbe kwamba ziko mashakani.
Bahari
baina ya Libya na Utaliano, ndio njia inayotumiwa kwa muda mrefu, na
wakimbizi kutoka Afrika na Mashariki ya Kati, ili kuingia Ulaya.BBC
Kati ya wahamiaji 264,500 Umoja wa mataifa unasema kuwa bahari ya Mediterranea ndio kivukio maarufu.
Kufikia sasa takriban watu laki moja wamewasili katika ufukwe wa Italia .
Manuari ya Kijeshi ya Norway ilikuwa imewaokoa wahamiaji 320 jumamosi asubuhi
Wengine zaidi ya laki moja u nusu 160,000 waliwasili Ugiriki.
Jarida
moja la Norway Aftenposten, limesema kuwa manuari ya kijeshi ya taifa
hilo Siem Pilot, liko njiani kuwasaidia wahamiaji hao walioko mashakani.
Manuari
hiyo iliwaokoa wahamiaji 320 mapema leo kabla ya kurejeshwa tena huko
huko kushiriki operesheni hii ya kuoko nafsi za watu wanaokisiwa kuwa
takriban 3,000.
Post a Comment