Tume ya
Taifa ya Uchaguzi Nchini Tanzania (NEC) imewahakikishia Watanzania wote
waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa
BVR kuwa watapiga kura.
Kaimu
Mkuu wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura Bi. Giveness Aswile
ametoa hakikisho hilo wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya
zoezi la uhakiki wapiga kura linaloendelea nchini nzima na kuongeza kuwa
hata wale ambao taarifa zao zilikosewa kwa bahati mbaya wakati wa
kuandikishwa watapiga kura na kuongeza kuwa kukosewa kwa taarifa zao
hakutawanyima sifa na haki yao ya msingi ya kupiga kura.
Bi.
Giveness amesisitiza kuwa pindi daftari la wapiga kura litakapo kamilika
vyama vyote vya siasa nchini vitapewa ili walitumie wakati wa kupiga
kura ili kuondoa wasiwasi wa kuwepo kwa wapiga kura wasio na sifa katia daftari hilo.
Post a Comment