Katika mchezo huo uliomalizika kwa Chelsea kushinda mabao 2-0 dhidi ya Arsenal, ulimalizika kwa Arsenal kuwa na wachezaji wawili pungufu waliooneshwa kadi nyekundu na mwamuzi Mike Dean.
Costa ambaye anakabiliwa na adhabu kwa mchezo mbaya kwa Koscienly alioneshwa kadi ya njano na mwamuzi Mike Dean ambaye hata hivyo haikujulikana kadi hiyo ni kwa kosa la Koscienly au ni majibizano yake na Gabriel Paulista ambaye pia alioneshwa kadi nyekundu baada ya kuingia katika mtego wa Costa.
FA pia wamempa adhabu Gabriel Paulista kwa kitendo chake kilichopelekea kupigwa kadi nyekundu, wakati Saint Carzola akipewa onyo kali, na klabu zote mbili za Arsenal na Chelsea zikipigwa faini kwa kutowafunza adabu wachezaji wake. Wote wamepewa hadi saa kumi na mbili jioni jumanne hii kukata rufaa.
CHANZO:SHAFFIH DAUDA
Post a Comment