Kuna mengi katika mchezo wa soka tumewahi kuyashuhudia mtu wangu lakini imezoeleka katika maisha ya kawaida kwa wachezaji, mfano ni kawaida kwa wachezaji soka kubadilishana jezi baada ya mchezo na kuna wakati Mbwana Samatta wa Tanzaniaaliomba kubadilishana jezi na Ahmed Musa anayekipiga CSK Moscow ya Urusi kama ishara ya kumbukumbu ya ukarimu wa Musa wakati wa majaribio yake CSK Moscow, tukio hilo lilitokea wakati Taifa Stars ilipokutana na Nigeria uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Neymar ameingia katika headlines baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya timu yake ya taifa ya Brazil dhidi ya Peru, mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 Urusi lakini Brazil iliibuka na ushindi wa goli 3-0 magoli ambayo yalifungwa na Douglas Costa, Renato Augusto, na Felipe Luis.
Baada ya mechi kumalizika Neymar aliona ni vyema kwenda kumpa zawadi ya jezi muamuzi wa mechi hiyo Jose Buitrago kutokea Colombia lakini muamuzi aliikataa jezi yaNeymar kitendo ambacho kinatafsirika kama muamuzi huyo aliogopa kuchukua kwa sababu huenda angeonekana kapendelea, lakini utamaduni wa kupata saini au jezi ya staa kwa watu wa nje ya Afrika ni kitu muhimu sana na wanaheshimu hivyo wengi walishangazwa kuona kapotezea kumbukumbu muhimu.
CHANZO:MILARD AYO
Post a Comment