KUMBUKUMBU.!
Mwaka 1995 katika uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi, Jimbo la Kigoma mjini, CHADEMA ilimsimamisha Dr.Amani Walid Kabourou ambaye alichuana vikali na Azim Premji wa CCM. Wagombea wengine ni Hussein Beji wa NCCR Mageuzi na Kashugu Anzaruni wa TADEA.
Baada ya uchaguzi Azim Premji (CCM) alitangazwa mshindi kwa kupata kura 16,692 dhidi ya Dr.Amani Walid Kabourou (CHADEMA) aliyepata kura 14,674. Hussein Beji (NCCR) alipata kura 192 na Kashugu Anzaruni (TADEA) akipata kura 39.
Baada ya matokeo hayo Kabourou akafungua kesi mahakama kuu kanda ya Tabora kupinga ushindi wa Premji. Wakili wa Kabourou alikuwa Marehemu Bob Makani ambaye kwa wakati huo alikuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA.
Baada ya kesi kusikilizwa pande zote ukafika wakati wa mawakili kuoneshana "umwamba" na uhodari wa vifungu vya sheria. Bob Makani akaomba ruhusa ya kutoka nje kwenda kuvuta sigara, Jaji akamruhusu. Akaenda akavuta sigara zake kisha akarudi ndani.
Alipofika akamuuliza Premji alipata kura ngapi. Premji akajibu 16,692. Makani akamuuliza tena una uhakika hizo ndio kura ulizopata? Premji akajibu ndio. Makani akamwambia "kwa hiyo unaidhibitishia hii mahakama kwamba wewe ni mtu makini?" Ptremji akasema ndio.
Makani akamuuliza unaweza kuniambia hilo lako ulilovaa lina vifungo vingapi? Premji akaanza kuhesabu "moja, mbili, tatu...."... Makani akamuambia Jaji kwamba "huyu mtu si makini, kama hajui idadi ya vifungo vya shati analovaa kila siku atawezaje kujua idadi ya kura zake?"
Kufikia hapo wanasheria wanasema "kesi ikawa imeisha".... Premji akatenguliwa ushindi wake na Kabourou akatangazwa kuwa mbunge wa Kigoma mjini 1996-2000.
The Law is not only about justice, but all about evidence and facts.!
Imepakuliwa Ukurasa wa Malisa Godlisten J.!
Post a Comment