Unknown Unknown Author
Title: KWA TULIO MBALI NA NYUMBANI:KISA CHA SIKIRI NA HADITHI YA MWANAMPOTEVU NINA KI DEDICATE KWENU!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kwa wanao penda kujisomea hadithi mbalimbali lazima watakua wamesha wahi kukutana na hadithi ya mwana mpotevu! Aliye omba sehemu y...

Kwa wanao penda kujisomea hadithi mbalimbali lazima watakua wamesha wahi kukutana na hadithi ya mwana mpotevu!

Aliye omba sehemu ya mali kwa baba yake ili imfae maishani,
Alipo pewa akaenda nchi ya mbali,
Huko akatapanya mali kwa kuendekeza starehe na anasa za dunia,

Haiyumukiniki MWANA MPOTEVU aliendekeza NGONO NA POMBE!
Akaishiwa fedha,
alitafuta kazi ya kufanya,
akageuka kijakazi,
huko alipata taabu hata akadiriki kula na nguruwe...

Akatafakari sana,
Akazingatia moyoni mwake,kwanini mimi napata taaabu?
Watumishi wengi kwa baba wanakula na kusaza...!
aka amua kurudi kwa baba yake!

Alipo karibia nyumbani kwao,akiwa mbali Baba yake alimwona mwanaye akija,
akamtambua tangu akiwa mbali....
aka mkumbatia,kisha,
Mtoto aka mwangukia baba yake na kumwambia 
...Nime kosa mbele ya nchi na mbele yako!
Nina omba nipokee Niwe  hata kijakazi wako,
Alipo mpokea alimfanyia sherehe,
Yule mwana aliye baki nyumbani alilalamika sana,
kwanini mwenzake afanyiwe sherehe kubwa vile ile hali alisha pewa sehemu yake ya mali na ame itapanya?

Baba yake,alimtuliza kwa kumwambia Huyu alikosekana hapa kitambo sasa,
Leo ame patikana kwanini nisimfanyie sherehe?

USI HOFU Mali yote hapa nyumbani ni Milki yako!! Alimsihi baba yule.
Naam:KWA TULIO MBALI NA NYUMBAN:TUSIENDEKEZE UVIVU,POMBE NA NGONO


JIKUMBUSHE NA HII YA SIKIRI

SIKILI MIMI MASIKINI, UVIVU WANGU NYUMBANI…
Sikili mimi maskini,
Uvivu wangu nyumbani,
Ukiwa huu njiani,
Nakufa hapa kwa nini?
Sadiki sasa ashiba,
Chakula kingi kwa Baba,
Nirudi tena kwa Baba,
Nakufa hapa kwa nini?
Naomba radhi nimekosa,
Nitakuwa mtoto mwema sasa,
Shambani tena sitakosa,
Baba na Mama nisameheni.
Nitalima kama Sadiki,
Nitalima wala sichoki,
Na nyumbani tena sitoki,
Baba na Mama nisameheni.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top