Unknown Unknown Author
Title: REJEA YETU LEO:NYERERE,SAMORA UMUHIMU WA KUJISOMEA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Imepakuliwa Kutoka Ukurasa wa Ado Shaibu, NYERERE, SAMORA NA UMUHIMU WA KUJISOMEA "Najua kuna wasomi wenzangu ambao sasa hawaso...


Imepakuliwa Kutoka Ukurasa wa Ado Shaibu,

NYERERE, SAMORA NA UMUHIMU WA KUJISOMEA
"Najua kuna wasomi wenzangu ambao sasa hawasomi kabisa. Nia yao ya kwenda shule ilikuwa kutafuta hati ambayo wangeweza kuitumia kama hirizi. Baada ya kuipata hati hiyo, kweli iliwapatia kazi, na sasa imetundikwa ukutani mahali ambapo kila mtu anaweza kuiona.
Lakini sasa hawasomi kabisa! Hili ni kosa kubwa sana linalotokana na mawazo ya kikoloni...
Basi huo ndio ujumbe wangu wa mwaka 1970. Kuishi ni kujifunza na kujifunza ni kujaribu kuishi zaidi. Basi katika mwaka mpya na tujifunze mambo mengi zaidi ili tuweze kuishi maisha bora..
Na tumwombe Mwenyezi Mungu atusaidie kuishi ili tujifunze mambo mengi zaidi juu ya maajabu yake katika ulimwengu huu tunamoishi na tujipatie faida za maisha hayo sisi wenyewe, watoto wetu na nchi yetu.
Nawakumbusheni tena ahadi moja ya TANU; nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote. Wananchi, nawatakia heri ya mwaka mpya".
Hii ni sehemu ya hotuba za Mwalimu Nyerere zilizo kwenye kijitabu chake kiitwacho "Elimu Haina Mwisho: Risala za Rais kwa Taifa alizozitoa kwenye mkesha wa mwaka mpya 1970-1971".
………………………………
"There are comrades who look down on study because they do not know its value. Study is like a lamp in the night which shows us the way. To work without studying is to advance in the dark. One can go forward, of course, but at great risk of stumbling or taking the wrong path…
Therefore, at this time when preparations are being made in agriculture for sowing the crops of the new season, we say to the comrades;
TO PRODUCE IS TO LEARN. LEARN IN ORDER TO PRODUCE AND STRUGGLE BETTER. ALUTA CONTINUA. INDEPENDENCIA OU MORTE (INDEPENDENCE OR DEATH!)
Hii ni sehemu ya maandiko ya Samora Machel yaliyokusanywa kwenye kitabu chake cha "Sowing the Seeds of Revolution". (uk 61-62)

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top