Unknown Unknown Author
Title: UCHAMBUZI RIPOTI YA CAG:UKWELI KUHUSU HALMASHAURI YA TUNDUMA NA HAI KUFANYA MADUDU!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na: Daniel Ezekiel Daniel   MALISA GODLISTEN Nimesoma na kuelewa hoja yako ya TUJISAHIHISHE. HOJA YAKO INA KASORO ...

MALISA GODLISTEN
Nimesoma na kuelewa hoja yako ya TUJISAHIHISHE. HOJA YAKO INA KASORO NYINGI................... NAOMBA NIKUSAHIHISHE.
Malisa GODLISTEN ni kaka yangu katika mambo ya uchambuzi, fikra na ni rafiki yangu sana.... Leo Nimesoma andiko lake lenye TITLE TUJISAHIHISHE.....
Malisa ametumia Ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali yaani Controller and Auditor General (CAG) kama msingi wa hoja yake ya TUJISAHIHISHE........
Ameeleza kwamba halmashauri zilizofanya vibaya katika ukaguzi wa CAG ni zile zinazoongozwa na ziliongozwa na chadema.................
Hoja hiyo sio ya kweli katika halmashauri ya Mji wa Tunduma..... Halmashauri ya Mji wa Tunduma ilikua chini ya chama cha mapinduzi kuanzia mwaka 2010 - 2015 na imekua chini ya chadema 2015-2020.... Madiwani wa chadema walikua wachache ukilinganisha na Madiwani wa ccm Mji wa Tunduma. Hivyo sio kweli kwamba chadema iliongoza Tunduma 2010-2015... Hiyo ni fallacy namba moja katika hoja ya Malisa. ........
Fallacy namba 2 ni kwamba, wakati wa ukaguzi wa Halmashauri Hai, Karatu na kwingine ilikua ni kipindi ambacho mabaraza ya Madiwani yalikua yamevunjwa tayari. Hivyo watendaji walifanya mambo kama wanavyotaka ikiwa ni pamoja na kificha vitabu vya ukaguzi kama Mji wa Tunduma nk. Hivyo Madiwani hawawezi kubeba lawama katika hilo... Fallacy namba mbili ya kutofanya uchunguzi au utafiti....
Malisa bado anaendelea kusema hajasikia Madiwani wakimuondoa mkurugenzi na watendaji wengine. Hii ni fallacy pia... Ukwel ni kwamba, baada ya kufunguliwa kwa baraza la Madiwani halmashauri ya Mji wa Tunduma la 2015-2020 Madiwani waliposoma na kufuatilia kwa kina yatokanayo na baraza lililopita, waliona uchafu mwingi sana katika taarifa ya baraza lililopita na waliazimia kumkataa Mkurugenzi mtendaji na watumishi wengine. Hivyo Madiwani wa chadema walifanya kazi yao na Simbachawene alimuondoa mkurugenzi katika mkutano wa hadhara Tunduma.......... Hii ilikua kabla ya Ripoti ya CAG. Hivyo si sahihi kubebesha chadema mzigo wa Tunduma.
Hata hivyo, Ripoti ya CAG ina mapungufu mengi sana hasa mapungufu ya uwasilishaji taarifa kwa lugha ya kiingereza na kiswahili... Ripoti baadhi ya maeneo katika Ripoti ya kiswahili inaonesha milioni kadhaa wakati kwenye Ripoti ya kiingereza inaonesha bilioni badala ya milioni. Kwa ushahidi soma Ripoti ya CAG ya kiingereza na kiswahili ya Halmashauri ya jiji la Tanga..... Hata hivyo, Ripoti hiyo inaonesha udhaifu mwingine kwamba shirika la NSSF hakuna ufisadi wakati Ripoti ya UTOH ya 2013/2014 inaonesha kuna ufisadi mwingi.... Halmashauri kama Mbogwe zilizofanya kazi ya kutoa rushwa ili kupata hati safi nazo zimepata hati yenye mashaka. Sasa unadhani nani anaamini Ripoti hiyo??? NSSF haina ufisadi???????
Malisa anaendelea kusema kwamba,, viongozi wakuu yaani aliyekua katibu mkuu DK slaa na mwenyekiti chadema taifa mh Freeman Mbowe wameaibisha taasisi. Binafsi Ripoti ya CAG ya huyu Prof Mussa Assard ninaiona ina mambo yasiona uhalisia. Kuna propaganda ndani yake kwa lengo la kudhoofisha upinzani...

Sasa Malisa alipojenga hoja zake za Tunduma kwamba ilikua halmashauri ya chadema na hakuna hatua dhidi ya wakurugenzi na watendaji nimepata ukakasi juu ya umakini wa kaka yangu Malisa GODLISTEN katika hoja zake kama zinafanyiwa utafiti wa kujitosheleza...
DANIEL EZEKIEL DANIEL
0628 244 784
danielezekiel2222@gmail.com

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top