Jana kwenye taarifa yaa habari ya ITV (saa 5 usiku), nimewaona madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru wakiongozwa na mbunge wao Comrade Josh Nassari wakiwa wamebeba nyundo na vifaa vizito - wakibomoa uzio uliojengwa na matajiri waliovamia na kujitwalia maeneo ya umma. Sote tunafahamu kuwa “uporaji wa ardhi’ unaofanywa na watu wenye “vipesa vyao” ni tatizo sugu. UJASIRI uliooneshwa na kina Nassari unapaswa kuigwa na halmashauri zingine. Siyo mnaamua vikaoni ati wananchi wakarudishe eneo lao, nendeni nyinyi wenyewe lirudisheni kwa mikono yenu, UONGOZI NI VITENDO!
Nassari anakumbuka sana tulipokuwa CHUO KIKUU, tukiamua jambo fulani sisi viongozi wa DARUSO ndiyo tungelikaa mbele kabisa na watawala wakija kuchukua hatua zinaanzia kwa viongozi, UONGOZI ni RISK na lazima uiishi kwa vitendo! Kwa mfano, siyo sahihi mnatangaza maandamano halafu viongozi mnabaki kwenye magari yenu. UONGOZI NI VITENDO, VITENDO, VITENDO!
Hongera sana Nassari.
Mtatiro J.Hongera sana Nassari.


Post a Comment