
News Feed
HEADING NZURI YA KUKUONGEZEA MAUZO UNAPOTANGAZA BIASHARA
Ulishawahi kuona tangazo lakini ukaishia kusoma heading na pengine hata hukuona umuhimu wa kuendelea kumalizia heading??
Makala hii italeta mapinduzi makubwa katika uandishi wa heading za matangazo yako ya biashara.
Kama utaandika makala au tangazo la biashara na watu wakaliona kisha wakalipita bila kulisoma, tatizo itakuwa ni heading (kichwa cha tangazo), heading itakuwa imeshindwa kutoa ushawishi kwa msomaji kuendelea kusoma utangulizi na yaliyomo.
Kuna mitindo mbalimbali ya kuandika heading zenye kumvuta msomaji na kumfanya aendelee kusoma utangulizi na hatimaye tangazo lote au makala yote.
Katika makala hii fupi, nitakusaidia njia moja ya uandishi wa heading ukiunganisha na njia zingine sahihi unapotangaza bidhaa au huduma, tangazo linakuwa na ushawishi mkubwa la kwa mteja kufanya maamuzi ya kulipia bidhaa au huduma yako.
Fatilia hapa:
KICHWA CHA TANGAZO KIHUSISHE JINA LA BIDHAA NA FAIDA ATAKAYO PATA MTEJA.
Mara nyingi watu hawanunui bidhaa unayouza, wananunua faida au matokeo yanayotolewa na bidhaa au huduma yako. Kama bidhaa au huduma yako inauwezo wa kusaidia watu unaowalenga katika biashara yako watakuwa tayari kulipia. Hivyo usitaje tu bidhaa na kuanza kuhimiza watu wanunue au walipie huduma na bidhaa zako unapotangaza.
Agalia mifano ifuatayo:
Mfano 1:
MAZIWA YA WATOTO
Heading ya kwanza, inataja tu jina la bidhaa haioneshi ni tatizo gani bidhaa inaweza kumsaidia mteja. Matangazo ya namna hii yapo mengi, kujitofautisha katika tangazo na kuonesha bidhaa yako ilivyo ya utofauti katika kumsaidia mteja kunaongeza ushawishi kwa mteja.
TUNAUZA MAGAUNI KWA SH. 50,000
Tangazo la pili unaweza kuona kama limekamilika lakini japo litakupa wateja pia litakufukuzia wateja wengi.
Pamoja na kosa la kutoonesha upekee wa gauni ambalo mteja atanufaika nalo, pia tangazo lina makosa ambayo hufanya mteja asiendelee kusoma tangazo baada ya heading. Mtengeneza tangazo ameweka hitimisho kabla ya kumshawishi mteja. Sentensi za lipia, toa gharama, na kiasi cha pesa ni vizuri yatumike baada ya kuwa umejenga ushawishi na ukaribu na mteja katika tangazo lako.
Pamoja na kosa la kutoonesha upekee wa gauni ambalo mteja atanufaika nalo, pia tangazo lina makosa ambayo hufanya mteja asiendelee kusoma tangazo baada ya heading. Mtengeneza tangazo ameweka hitimisho kabla ya kumshawishi mteja. Sentensi za lipia, toa gharama, na kiasi cha pesa ni vizuri yatumike baada ya kuwa umejenga ushawishi na ukaribu na mteja katika tangazo lako.
JIPATIE SIMU YA XXX.
Tangazo la tatu, lina makosa kama tangazo la kwanza. Simu zipo nyingi na makampuni tofauti, usiishie tu kutaja simu ya kampuni flani au jina la simu. Onesha utofauti uliopo kati ya simu yako na zingine, utofauti unaogusa hitaji la mteja ambaye umelenga kumsaidia kutimiza ndoto yake ya kuwa na simu kama unayo uza. Vinginevyo anapita simu yako aende kutafuta kwingine japo anataka simu yenye sifa kama yako unayouza.
(linganisha mifano ya 1 na mifano inayofuata, mifano 2)
Mfano 2:
MAZIWA YA MTOTO YENYE VIRUTUBISHO P & Q NI MAZURI KWA AFYA YA MTOTO.
Tangazo hili limetaja bidhaa inayouzwa na faida ya bidhaa kwa mteja, ikiwa Virutubisho vilivyo tajwa watu walio lengwa wana uhitaji, hawatasita kununua. Baada ya heading nzuri kinachotakiwa ni mbinu za kumsaidia mteja aone umhimu wa kuwa na maziwa hayo kwa mtoto.
JIPATIE APPLICATION INAYOKUWEZESHA KUNASA MAWASILIANO YA MPENZI WAKO.
Tangazo hili la pili, limetaja bidhaa (japo jina halisi halijawekwa wazi) lakini kikubwa limetaja matokeo au manufaa atakayopata mteja. Pia mwandaaji wa tangazo anafahamu mteja wake ni nani ndio maana ametaja mawasiliano ya mpenzi wako, kwa sababu anafahamu wateja wake wakubwa nambari moja ni watu walio katika mahusiano. Hivyo amewalenga moja kwa moja.
Sio siri, unapoandika tangazo linalo taja matokeo au faida atakayopata mtumiaji na kisha tangazo ukalifiksha kwa wahitaji, kama baada ya heading utaweza kumshawishi mteja, uwezekano mkubwa wa kuuza utakuwepo.
Nikupe mfano halisi kuhusu heading; nimekuwa nikitafuta njia rahisi ya kutumia namba zangu za simu zote mbili katika, “Wasap” kwa kutumia simu moja. Njia ya kwanza niliopata ilikuwa ndefu na inahitaji ku_root simu, mimi sikuipenda njia hii.
Badae niliona tangazo “DOWNLOAD (........) BURE, TUMIA WASAP MBILI KATIKA SIMU YAKO” msomaji fikri kidogo kuhusu kilichotokea.
Je unahisi niliacha kudownload........ nilidownload haraka, kwa nini nili Download?
Kwa sababu, kwanza tangazo lilinifikia nikiwa nina uhitaji wa kutumia namba mbili wasap katika simu moja. (hapa unapotangaza zingatia wahitaji wa bidhaa au huduma)
Pili nili Download kwa sababu tangazo lilijieleza wazi nikidownload nanufaika nini (hapa unapotangaza zingatia kujumuisha faida kwa mteja katika heading kama faida zipo nyingi unaweza kuandika matangazo tofauti tofauti au tangazo moja faida zingine utaelezea katika tangazo) isingekuwa kuona faida katika heading ningelipita tangazo.
Hii application wengi wanaitumia, kati ya watu watano (8) walio install katika simu zao kwa kuona tangazo, niliwauliza wamejuaje kuwa inawezesha kutumia watsap mbili (2)?
Jibu lilikuwa, heading. Wakati wanaperuzi mtandaoni wakaona neno Download utumie watsap mbili.
Jibu lilikuwa, heading. Wakati wanaperuzi mtandaoni wakaona neno Download utumie watsap mbili.
ZINGATIA HEADING YA TANGAZO LA BIASHARA KUONGEZA MAUZO.
#ShoriMN (Online Marketing Coach)
WhatsApp: 0682 937 214
Email: success@shorisuccesslife.com
Email: success@shorisuccesslife.com
Post a Comment