Ifuatayo ni baadhi ya miti maarufu Tanzania iwe ili pandwa au ilijiotea yenyewe.Baadhi ya miti imekuwa kivutio kutokana na historia na faida yake kwa jamii.Miti ni viumbe hai vinavyojumuisha uzito hai kama ilivyo kwa wanyama na uhai wake ni muhimu kwa dunia endelevu.Miti imechangia katika dhima mbalimbali iwe historia ,elimu,utamaduni,harakati na utalii.Miti ifuatayo ni maarufu kutokana na kuvutia watalii,wasomi na watu wadini na wa matambiko kutoka maeneo tofauti Tanzania na dunia kwa ujumla.
Mdegree Tree (FICUS)
Mti huu unapatikana katika chuo kikuu cha Dar es Salaam ni mti maarufu uliopandwa mwaka 1960 na raisi wa kwanza wa Tanzania Mwl J.#Nyerere.Mti huu ulioko mbele ya ukumbi wa Nkuruma hall unaopatia wanafunzi kivuli cha kusoma na kupata degree zao.Mahali pa mti huu ndipo harakati za maandamano na migomo ya wanafunzi huanzia.Mahali hapa pa mti huu pana mazingira mazuri ya kusomea pamoja na mtandao wa bure.
Mwembe waliokutana Dr David Livingstone na Stanley
Mwembe huu ulioko #Ujiji #Kigoma karibu na jumba la makumbusho la #DrLivingstone ndipo walipokutana wachunguzi karne ya 19.Mwembe huu uko chini ya idara ya Mali kale kama kumbukumbu ya historia ya bara.Mwembe huu mpaka leo umesimama na kuvutia watu mbalimbali duniani.
Mbuyu wa kujificha Majangili (poachers hide)
Mti huu aina ya mbuyu(Adansonia digitata) unapatikana katika hifadhi ya taifa Tarangire.Hapo zamani mbuyu huu ulikuwa unatumika pango la kujificha majangili waliokuwa wanawinda wanyamapori ndani ya hifadhi.Mbuyu huu katikati unapango ambalo wanaweza kuingia takribani watu arobaini.Mbuyu huu unavutia watalii wanaotembelea hifadhi ya #Tarangire na ni mojawapo ya rasilimali ya utalii inayopatikana katika hifadhi ya Tarangire.
Mbuyu wa kanisa
Mti huu ni maarufu na muhimu kwa kanisa katoliki na historia yake ya kuenea kwa ukiristo Afrika Mashariki.Mbuyu huu unaopatikana katika mji mkongwe wa #Bagamoyoulipandwa mwaka 1860 na padri Anthony Horner kwa misheni ya Katoliki Bagamoyo.Mti huu jinsi unavyokuwa kwa Wakatoliki ndo jinsi imani ya Kanisa Katoliki linavyoenea Afrika Mashariki.Mti huu una baki ya mjororo uliokuwa unatumika kufunga punda wa muuguzi Madame de Chevalier mnamo mwaka 1895.
Mvule wa Ajabu
Mvule wa Ajabu ni mti maarufu unaopatikana katika hifadhi ya msitu wa Rau #Moshiinasemekana na Tanzania Tourist Board kwamba ndo mvule wenye umri mrefu#Afrika.Mti huu wenye umri takribani miaka 194 umeweza kudumu umri huu katikati ya miti mingi muhimu ya mbao na sgughuli za binadamu kutokana na mila na desturi za wananchi wanaozunguka msitu huu.Historia inayo kwamba mti huu ulikuwa ukikatwa unatoa damu pamoja na shughuli za matambiko mti huu ukapona na kutimiza umri mrefu kati ya miti ya mivule Tanzania.Hii inaonyesha kwamba mila na desturi zetu za Mwafrika zilikuwa zinasaidia kuhifadhi mimea na wanyama toka kale.Mti huu ni rasilimali ya utalii katika #Msitu wa Hifadhi Rau.ndio maana Rau Rau eco and cultural tourism programme wanaendeleza mpango wao mahsusi wa utalii ikiwa kivutio kikubwa ni Mvule wa Ajabu.
Hii ni baadhi ya miti maarufu michache inayopatikana #Tanzania na ipo katika uhifadhi uwe wa Mali Asili au Mali Kale.Makala ni maalumu kwa kutambua michango miti katika historia,tamaduni na maisha yetu ya kila siku.Mimi ni Mkumbatia Mti #TREEHUGGER
Credit:Eco Footprints Tz,
Post a Comment