Unknown Unknown Author
Title: REJEA YETU LEO:TULIPO KUTANA MARA YA MWISHO.....!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
NENO LA LEO: TULIPOACHANA MARA YA MWISHO...! Ndugu zangu, Sir Rider Hagaard katika kitabu chake, ' Machimbo ya Mfalme Suleim...
Ndugu zangu,
Sir Rider Hagaard katika kitabu chake, ' Machimbo ya Mfalme Suleiman', anaaandika; kuwa Allan Quaterman alipokuwa na wenzake Sir Henry na Bw. Good , walisafiri wakitafuta wapagazi, basi, walifika kwa balozi wa mji wa Lamu.
Allan Qaterman na wenzake walitafuta wapagazi maana walikuwa wakiitafuta nchi ya watu weupe na isiyojulikana. Wakiwa Lamu walimwona Umsolopagazi akiwa na wenzake kwenye hali ya upagazi.
Allan Quaterman akatamka;
"Tulipoachana mara ya mwisho ulikuwa ni mfalme katika taifa la Wazulu, ona, watu wale ingawa ni jasiri, lakini, walipokuwa wakizunguuka mioto nyakati za usiku walikuwa wakisimulia habari za ujasiri wako.
Je, ni nini kilichokuangusha ewe Umsolopagazi?"
Umsolopagazi akajibu;
" Eeh baba, mwanamke alinihaini mahutini , akalifunika jina langu kwa aibu.
Ndiye yeye mke wangu mwenyewe, mwanamwali mwenye uso kama mwezi"
Allan Quaterman akasema;
"Ama, ni kweli jambo la fedheha, kwa jasiri kama wewe kuangusha himaya yako kwa sura ya mwanamke"
Ni nini basi adili ya jambo hili?
Mtazamo wangu kama mwandishi; Hakuna fedheha ya kupenda. Hivyo, hakuna dhambi ya mapenzi wala kupenda. Hapa basi namtetea Umsolopagazi, ingawa, katika lililomtokea, alipaswa kutambua, kuwa katika dunia hii mtihani una matokeo mawili; kufaulu na kuanguka. Duniani hakuna sare ya mtihani. Kwa kila jambo ulipendalo, hupaswi kulipenda ukajisahau, na hata kushindwa kutimiza wajibu wa kutekeleza majukumu yako.
Imah, mwanadamu uitafute adili na kiasi. Maana, kila jambo kiasi.
Ni Neno la Leo.
Maggid,
Iringa.

TAFAKURI YA MJUMBE:
Nime jikuta nikivutiwa na wasaa huu,
Ni maneno yanayo Fikirisha sana....

Lakini kuna jambo la kujifunza pia.

Anguko lako linapo changiwa na Mwanamke Umpendaye,

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top