Ni karibu siku 12 kabla ya uchaguzi mdogo wa ubunge wa Jimbo la Kalenga, zimeanza kuonekana dalili za vitendo vya uvunjifu wa amani baada ya vyama vikuu viwili vinavyokabana koo – CCM na Chadema kuanza kutuhumiana kwa vurugu.
Kutokana na hali hiyo, hofu imetanda miongoni mwa
wakazi wa Kalenga kutokana na madai kuwa kila chama kimeingiza watu
kutoka nje ya Mkoa wa Iringa kwa lengo la kufanya vurugu kwenye mikutano
ya kampeni.
Madai ya Chadema
Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo, Benson
Kigaila aliwaambia waandishi wa habari kuwa walinzi wa chama hicho juzi
walimkamata mtu mmoja aliyetaka kuchoma moja ya ngome zao zilizopo
katika kata 13 za Jimbo la Kalenga.
Kigaila alisema mtu huyo ni miongoni mwa watu
walioletwa na CCM kutoka mikoa mbalimbali ikiwamo Arusha na Dodoma na
kwamba watu wengine kwa kazi hiyo jana walikuwa njiani kutoka Mwanza.
“Tumeweka ngome katika kata zote 11 za Jimbo la
Kalenga na leo alfajiri (jana) vijana wa CCM walikuja kufanya vurugu
kwenye kambi yetu ya Wassa, baada ya mvutano, vijana wetu walifanikiwa
kumkamata mmoja wao na taarifa zake zimefikishwa polisi,” alisema
Kigaila.
Pamoja na kukamatwa kwa kijana huyo, Kigaila
aliwatuhumu wafuasi wa CCM kwa kufanya vurugu, kushusha bendera za
Chadema na kuchana picha za mgombea wake, Grace Tendega.
“Tuna ushahidi wa mambo mengi na kesho (leo)
tutaweka bayana kila kitu kilichofanyika, na majina ya wahusika wake.
Tunataka polisi wafanye kazi yao kuhakikisha wanalinda amani iliyopo,”
alisema .
Kigaila alidai vijana wa Green Guard wa CCM kutoka
Arusha wakiongozwa na kijana aliyedai anajulikana kwa jina maarufu la
Mjusi, tayari wamepiga kambi Ifunda, na kwamba wengine watatu kutoka
Mwanza walianza safari yao jana kwenda Kalenga kwa kutumia usafiri wa
gari aina ya Toyota Noah.
Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga alikanusha tuhuma kuwaleta vijana kutoka mikoa mingine kufanya vurugu Kalenga.
Shutuma za CCM
CCM nao wamekituhumu Chadema kuwa kimeleta watu
wenye silaha na tindikali kutoka nje ya Mkoa wa Iringa kwa ajili ya
kufanya fujo kwenye uchaguzi na kuwadhuru wananchi na wana-CCM jimbo la
Kalenga.
Na Mjumbe Jr
Mbozi
Post a Comment