Unknown Unknown Author
Title: JESHI LA URUSI LARUHUSIWA KWENDA CRIMEA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Bunge la Urusi limeidhinisha ombi la Rais Putin kuwa wanajeshi wa Uru...

Bunge la Crimea linapepea bendera ya Urusi
Bunge la Urusi limeidhinisha ombi la Rais Putin kuwa wanajeshi wa Urusi watumike Ukraine.
Wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Urusi imesema hiyo haimaanishi kuwa wataanza kutumika moja kwa moja, ingawa wakuu wa Ukraine wanasema Urusi imeshatuma wanajeshi 6,000 zaidi huko Crimea.
Kikosi cha wanamaji wa Urusi katika Black Sea kimesema kuwa wanajeshi wake wanapiga doria pamoja na wenyeji wa Crimea wanaounga mkono Urusi, ili kulinda vituo vyake.
Mwandishi wa BBC alioko Sevastopol anasema wanajeshi wanaonekana zaidi.
Meli za Ukraine za kulinda pwani zimeondoka kuepuka kuchukuliwa na Urusi na mwandishi wa BBC anasema kuna hisia kuwa ras wa Crimea inazidi kuwaponyoka wakuu mjini Kiev.

CHANZO:BBC SWAHILI
Na Mjumbe Jr
Mbozi

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top