Wazir wa elimu na mafunzo ya ufundi Dk Shukuru Kawambwa
Serikali imesema kuwa pamoja na matokeo yakidato cha nne kuonesha hakuna shule zake katika 10 bora,hali ya ufaulu ni nzuri na haupishani na shule sizizo za serikali.
Waziri wa elimu na Mafunzo ya ufundi, Dk Shukuru kawambwa pamoja na naibu waziri wake mh. Jenista Mhagama walitoa ufafanuzi huo kwa waandishi wa habari jana mjini Dodoma.Waziri alisema kutofautiana kwa matokeo hayo kunatokana na kwamba shule hizo binafsi huchukua watoto wanaofanya vizuri zaidi katika elimu ya msingi kuliko za serikali.
Dk Kawambwa alisema wakati mwingine shule hizo binafsi huwafanyisha mtihani wa mchujo na kusajili wanafunzi wa kidato cha kwanza kabla hata serikali haijatoa matokeo ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.
Akisisitiza kutotofautiana kwa matokeo hayo waziri alitoa mfano wa shule za Ilboru,Kibaha,Mzumbe na Tabora wavulana kwamba hazina wanafunzi waliofeli katika daraja la sifuri
Wakati huohuo Kawambwa amesema mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN)umechangia kwa kiwango kikubwa kupanda kwa ufaulu.
Na Mjumbe Jr
Mbozi.
Post a Comment