Unknown Unknown Author
Title: DROO YA CAF 2015 YATANGAZWA;TAZAMA MAKUNDI YOTE NA TIMU ZAKE HAPA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Droo ya Afcon2015 yatangazwa Droo ya Kufuzu kwa kombe la mataifa bingwa Barani Afrika mwakani{ Afcon} imefanyika huko cairo Misri h...

Droo ya Afcon2015 yatangazwa

Droo ya Kufuzu kwa kombe la mataifa bingwa Barani Afrika mwakani{ Afcon} imefanyika huko cairo Misri huku timu zote za kanda ya Afrika Mashariki zikiratibiwa kucheza katika mechi za mchujo kabla ya kushirikimechi za kufuzu .
Kenya itachuana dhidi ya Visiwa vya Comoro ,Tanzania ipambane na Zimbabwe, Uganda imeratibiwa kutoana kijasho dhidi ya Madagascar nayo Rwanda ikivaana na Libya.

Raundi ya Kwanza

  • Liberia v Lesotho
  • Kenya v Comoros Islands
  • Madagascar v Uganda
  • Mauritania v Equatorial Guinea
  • Namibia v Congo
  • Libya v Rwanda
  • Burundi v Botswana
  • Central African Republic v Guinea Bissau
  • Swaziland v Sierra Leone
  • Gambia v Seychelles
  • Sao Tome e Principe v Benin
  • Malawi v Chad
  • Tanzania v Zimbabwe
  • Mozambique v South Sudan
Burundi kwa upande wake itachuana dhidi ya Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikiratibiwa kuvaana na Namibia.
Baada ya kushiriki mkondo wa kwanza wa maondoano mataifa hayo tena yatalazimika kuchuana miongoni mwao ilikufuzu kwa awamu ya pili .
Mshindi wa mkondo huo wa pili ndio watakaojumuishwa katika makundi saba yaliyotajwa jana.

Raundi ya Pili

Liberia or Lesotho v Kenya or Comoros Islands
Madagascar ,Uganda v Mauritania ,Equatorial Guinea
Namibia , Congo v Libya , Rwanda
Burundi , Botswana v CAR , Guinea Bissau
Swaziland or Sierra Leone v Gambia , Seychelles
Sao Tome e Principe or Benin v Malawi , Chad
Tanzania , Zimbabwe v Msumbiji , Sudan kusini
Mechi za raundi ya kwanza zitangoa nanga tarehe 6-18 Mei.
Mechi za marudio zitasakatwa wikiendi ya tarehe 30-31 Mei hadi Juni Mosi .
Katika mechi zitakazoibua hisia ni pamoja na mabingwa watetezi Nigeria ambao wameratibiwa kuvaana na Afrika Kusini.
Mahasimu wa jadi kaskazini mwa Afrika Tunisia na Misri wameratibiwa kukwaruzana nayo Ghana,ikitoana kijasho na Togo.
Aidha Ivory Coast itafungua kampeini yake ya kufuzu kwa dimba hilo lenye hadhi barani dhidi ya mahasimu wao wakuu Cameroon.
Droo ya Makundi:
Kundi A :
Nigeria,
Sudan,
South Africa
{Namibia vs Congo Brazzaville/Libya vs Rwanda}
Kundi B :
Mali,
Ethiopia,
Algeria
{ Sao Tome e Principe vs Benin/Malawi vs Chad}

 
Kundi C:
Burkina Faso,
Gabon,
Angola
{ Liberia vs Lesotho/Kenya vs Comoros Islands}
Kundi D:
Ivory Coast,
Democratic Republic of Congo,
Cameroon
{ Swaziland vs Sierra Leone/Gambia vs. Seychelles}
Kundi E:
Ghana,
Guinea,
Togo
{Madagascar vs Uganda/Mauritania vs Equatorial Guinea}
Group F:
Zambia,
Niger,
Cape Verde Islands
{ Tanzania vs Zimbabwe/Mozambique vs South Sudan}
Kundi G:
Tunisia,
Senegal,
Egypt
{ Burundi vs Botswana/ Central African Republic vs Guinea Bissau}
Mechi za makundi zitaandaliwa kati ya tarehe 5-6 Septemba na tarehe 10 Septemba.
Mkondo wa pili utaandaliwa kati ya tarehe 14-15 November na 19 November.
Washindi wawili katika kila kundi watajiunga na wenyeji Morocco mwakani kwenye kipute cha kuwania taji la taifa bingwa barani Afrika 2015.

MJUMBE Sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top