Unknown Unknown Author
Title: UME SIKIA HII?? CHORUS YA WIMBO WA PROFESA JAY "KIPI SIJASIKIA" ILI MTOA MACHOZI DIAMOND WAKATI ANAITENGENEZA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
the QUARTZ Blog Wimbo wa Profesa Jay aliomshirikisha Diamond Platinumz ‘Kipi Sijasikia’umepokelewa kwa hisia na mas...
the QUARTZ Blog




Wimbo wa Profesa Jay aliomshirikisha Diamond Platinumz ‘Kipi Sijasikia’umepokelewa kwa hisia na mashabiki wengi ambao wengi wao wameguswa na ujumbe na kuuhusisha na kile kilichowahi kuwatokea wao.

“Ngoma hii ya Kipi Sijasikia alinipigia Mboni Masimba na Lady Jay Dee pia, Lady Jay Dee aliniambia ‘Jay exactly umeniimbia mimi’. Mboni Masimba alinaambia Jembee (ananiitaga Jembe) hii ngoma sasa umeamua kuniimba kabisa. Na sio hao tu...hao ni watu maarufu ambao wamenipigia lakini watu wengine wananiambia mtaani kwamba huu wimbo unawahusu kwa sababu hayo ndio maisha tunayoyaishi.” Alisema Profesa Jay wakati anafanya mahojiano na Fred ‘Fredwaa’ Fidelis katika kipindi cha Sun Rise cha 100.5 Times Fm.
Lakini kiitikio cha wimbo huo pia kinaongeza hisia kali kwa watu ambao ujumbe unawahusu kwa jinsi ambavyo kimeimbwa na Diamond Platinumz. Diamond aliguswa na wimbo huo tangu akiwa studio na akashindwa kuzuia hisia zake.
Profesa aliiambia Sun Rise ya Times Fm kuwa wakati Diamond anarekodi chorus hiyo alikuwa analia kutokana na kuguswa na ujumbe wa wimbo huo pamoja na kufanya kazi na wakongwe Profesa Jay na producer Majani.
 “Lakini kilichotushangaza alipoingia booth ili arekodi chorus Diamond alikuwa anaimba huku analia. Sisi tuko kwenye monitors huku tunamuangalia jamaa upande wa pili kwenye booth tunamuona Diamond analia. Alikuwa imotional unajua ile...ilimgusa sana. Sisi tulikuwa tunashangaa mimi na Majani ‘huyu jamaa analia nini?’
“Lakini baadae tulimuuliza alituambia ‘nimefurahi sana katika maisha yangu kufanya kazi na Profesa Jay pamoja na Majani, hilo moja. Lakini pili, mlivyoimba humu ndani vyote vinanihusu mimi…vimenitokea sana katika maisha yangu na changamoto zote hizo’..so yale ndio yalitokea studio. Kiukweli hii ngoma ilikuwa blessed tangu studio na kila mtu alikuwa anasema ‘yeah men it’s on’.” Ameeleza Profesa Jay.
MJUMBE Sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top