Unknown Unknown Author
Title: FLOYD MAY WEATHER ....! MCHEZA MASUMBWI BORA DUNIANI ASIYE ISHIWA MAJIGAMBO!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Huko mbele kwa wenzetu MAJIGAMBO Ukisha fanikiwa ni sehemu ya Utamaduni wao! Yaani kila anaye Fanikiwa kutoka kimaisha Lazima ajitangaz...
Huko mbele kwa wenzetu MAJIGAMBO Ukisha fanikiwa ni sehemu ya Utamaduni wao! Yaani kila anaye Fanikiwa kutoka kimaisha Lazima ajitangaze kwa namna moja amanyingine.
Nahii huwapa Changmoto na Hamasa kubwa wengine kufanya kazi kwa bidii na Maarifa ili nao Siku moja wafikie ndoto zao na wazi dhihirishe mbele ya jamii yao.
Mgari ya Kifahari Anayo Miliki Mcheza masumbwi Bora Duniani Floyd Mayweather!
Siku alipo ya nunua Aliandika "Hivi ni Vi Toy Vyangu nilivyo amua kuwa navyo..."

MAJIGAMBO ni Moja ya Utamaduni mzuri kimaisha kwani mtu anaye jingamba daima ataweka malengo yake chanya hai ili siku zote ile legacy yake iishi,hata siku akisha pumzika kwa Amani.
Ni moja ya Utamaduni Mzuri na Ninao Upenda sana!
Utamaduni huu wa majigambo kwa wenzetu ni Tofauti na utamaduni wetu ambapo mtu akisha fanikiwa hujifanyisha masikini,Huigiza Maisha ya kimasikini kabisa hata kufikia hatua ya kuweza kutembea Peku wakati Ana miliki Duka la Jumla la Viatu! Ili awafariji na Kuwapumbaza majirani zake wazidi kujisahau na kujiona wako sawa tu! Hawana Tofauti.

Kuna Bosi wangu mmoja Nime wahi kukutana naye mazingira flani ya kazi ana eneza hulka hiyo na kuitukuza,Hulka ya Kilaghai na kitapeli ndani ya jamii.Kwake hata Kuvaa tai ni mwiko kuingia Ofisini mwake... Usiongelee kuvaa Suti! Utaitwa na Utapewa Barua ya Onyo.Huu ni Upuuzi na kufanya hivi ni kukubali upuuzi.
Nakumbuka Miaka flani ya nyuma kidogo nikiwa nafanya kazi na bosi wangu yule kuna vijana wanao soma Elimu ya juu katika vyuo tofauti tofauti nchini;walijikusanya wakafunga safari ili waje wawahamasishe wadogo zao wano Soma shule mbali mbali wilayani pale kwa kujieleza jinsi walivyo fanikiwa kufikia pale walipo! Kwakuwa walikuja na baraka za kiserikari ili mlazimu awapokee tu kwa shingo upande.Jamaa walipewa jukwaa wakalitumia kweli kweli,na wengine wali muzidi hata Benjamin Carson yule wa THINK BIG! Hata ROBIN SHARMA hawa fikii.Moyoni nikasema wow! Zats it.Kama vijana hawa wange fanya hivi mara kadhaa ama kama utamaduni wao jamii inge waelewa na madoga wengi wange hamasika sana.

 Private Jet ya Timu nzima ya Floyd May weather;aikiwa ameshatua Afrika Kusini

Kumbe Bosi ili hulka ya wale vijana kuelezea jinsi ya kufanikiwa kwa wadogo zao ili mkera saba mara sabini,na hakuificha hii baada ya jamaa kuondoka ikabidi aanze kuwapiga vijembe,jamaa! Nakwakua sisi wengine hatuna simile tulimweleza wazi kuwa vijana wana nia nzuri tu na sio kama unavyo taka kuwa tafsiri wewe,wao wana wahamasisha/wana tuhamasisha.Ni sisi kuamua tufanyeje ili siku moja tufikie pale walipo! ili nilazimu nivunje ukimya na nimweleze wazi wazi maneno amabayo nina amini hakutaka kuyasikiliza na hapendi kuyasikia!
Huu ni Utamaduni wa KISHIRIKINA.... Huu ni Ujinga.... Huu ni Ulaghai.... Huu ni Utapeli....! Utamaduni kama huu niutamduni usio na Tija kwetu na kwa vizazi vyetu vijavyo.Ili kuongeza Ufanisi wa Fikra zetu na matamanio ya kufikkia Malengo flani  ninge pendekeza na sisi Tuufufue ule Utamaduni wetu wa Zamani wa MJIGAMBO,Hata ikibidi tuji pige pige na vifuani mwetu pale tunapo yaelezea mafanikio yetu kwa wengine wanao yatamani na kutaka kujifunza kutoka kwetu.
Huyu jamaa Picha ni Anaitwa Floyd May weather nadhani ndiye mcheza masumbwi bora duniani kwa sasa.
Haishiwi maneno... Jamaa huyu nadhani mtaani kwake ndiye anaongoza kwa MAJIGAMBO! Sisemi huko mbele kwa wenzetu hakuna wengine,Hapana! Wapo wengi sana Kwa kuwataja wachache tu ni kama vile akina Jay Z wa BEYONCE,Bird Man wa CMB,Pi Diddy wa BAD BOYZ na wengine wafanyao hayo kwa ajili ya jamii yao na Taifa lao pia.
SALUTE SANA.

MJUMBE sr
Near Mbeya

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top