Unknown Unknown Author
Title: HII HAPA SIO KALAMU KAMA UNAVYO IONA NI SILAHA YA KIITERIJENSIA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Bastola ya kalamu aina ya Stinger (tamka ‘Sting’a’) ni silaha ‘halali’ kwa matumizi ya kawaida ya binadamu huko nchini Marekani hadi ...


Bastola ya kalamu aina ya Stinger (tamka ‘Sting’a’) ni silaha ‘halali’ kwa matumizi ya kawaida ya binadamu huko nchini Marekani hadi hii leo; halali kwa maana ya ATF – Shirika la Pombe, Tumbaku na Silaha la Marekani – kuichukulia kama silaha ya kawaida. Lakini Stinger ya John Murphy haikuwa (wala haijawahi kuwa) silaha ya kawaida! Ilitengenezwa kwa ajili ya matumizi ya Idara ya Usalama ya Tume ya Dunia (WIS – ‘WODEC Intelligence Services’) na kwa ajili ya matumizi ya Kikosi cha Kikomandoo cha Tume ya Dunia (EAC – ‘Executive Action Corps’). Stinger ya Murphy ilikuwa na uwezo wa kubeba risasi moja ndogo kwa wakati mmoja – iliyokuwa na ukubwa wa inchi 0.22 ya mtutu wa bunduki (‘.22 caliber’) – na kidonge kimoja cha ‘cyanide’ (‘potassium suicide pill’): ili akitekwa akimeze na kufa; kuliko kutoboa siri za EAC, na siri za Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya. Aidha, Stinger ya Murphy ilikuwa na uwezo wa kufyatua risasi ikiwa imenyooka (Stinger ya kawaida hufyatua risasi ikiwa imejikunja) na kifyatulio chake kilikuwa kwenye kichwa cha kalamu; na ilikuwa na koki mbili: moja kwa ajili ya risasi, na nyingine kwa ajili ya mrija wa kalamu, tofauti na Stinger ya kawaida ambayo ina koki moja, mbele ya kifyatulio. Stinger ya Murphy ilikuwa na uwezo wa kuandika kama kalamu ya kawaida! Ilikuwa na uwezo wa kutumia kiwambo cha kupunguza sauti, kama Stinger za kawaida.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top