Unknown Unknown Author
Title: IMANI ZA KISHIRIKINA ZAKWAMISHA MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
BAADHI ya Wananchi Katika Kata ya Liganga Songea Vijijini Mkoani Ruvuma wamekuwa na Imani potofu wauguapo Maralia hivyo elimu ...



BAADHI ya Wananchi Katika Kata ya Liganga Songea Vijijini Mkoani Ruvuma wamekuwa na Imani potofu wauguapo Maralia hivyo elimu ya Ugonjwa huo bado ni changamoto Vijjini.
Hayo yameelezwa na Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Ernest Haule wakati akizungumza katika Siku yaZMaralia iliyoandaliwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika Shamba la Kahawa la Kampuni ya Aviv Tanzania LTD.
'Elimu ya Maralia Hapa ni changamoto na kutokana na hali hiyo ndio maana tumeamua kuandaa siku hii ya Maralia kwa kushirikiana na Kampuni ya Aviv katika Kata hii ya Liganga'anasema Mtendaji huyo na kuongezaMaralia ni Ugonjwa wa kawaida hivyo Wananchi wanapaswa wanapojisikia dalili za Maralia kuwahi kupima na kupatiwa matibabu badala ya kuamini ushirikina.
Kwa upande wake Msimamizi wa Shamba hilo la Kahawa kutoka Kampuni ya Aviv Tanzania LTD Amilt Kumar amesema kuwa wameandaa Siku hiyo ambayo huadhimishwa kila Aprili 25 kwa Wafanyakazi 1000 Zkushindwa kufanya Shughuli zao sawasawa. 
Chanzo;Mjengwa
Mjumbe Jr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top