Unknown Unknown Author
Title: MAFURIKO YAUA KYELA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Watu watatu wamefariki dunia na wengine watatu hawajulikani walipo baada ya kukumbwa na mafuriko yaliyotokea katika maeneo ...



Watu watatu wamefariki dunia na wengine watatu hawajulikani walipo baada ya kukumbwa na mafuriko yaliyotokea katika maeneo mbalimbali wilayani Kyela mkoani Mbeya.

Mafuriko hayo pia yamesababisha shule 27 kufungwa zikiwamo 20 za msingi na saba za sekondari kutokana na kuzingirwa na maji.

Mafuriko hayo pia yamezoa daraja la kamba linaloelea (kiteputepu) katika Mto Kiwira, linalounganisha kata za Ndandalo na Ibungu na kusababisha wananchi kukosa mahitaji mbalimbali, hivyo kulazimika kuomba boti.

Athari nyingine zilizotokana na mafuriko hayo ni kukatika kwa mawasiliano katika barabara inayounganisha Kikusya - Kyela – Ipinda hadi Matema na kufungwa kwa barabara ya kwenda Bandari ya Itungi katika Ziwa Nyasa.
MJUMBE Sr 
MBEYA

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top