Unknown Unknown Author
Title: SHILINGI 2,000 ZILINIONZA NIKAIBIWA MTOTO.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mboka akiwa na mtoto wake baada ya kukabidhiwa na polisi.  Na Godfrey Kahango, Mwananchi Posted  Jumanne,Aprili29  2014  saa 10:...
Mboka akiwa na mtoto wake baada ya kukabidhiwa na polisi. 
Na Godfrey Kahango, Mwananchi

Posted  Jumanne,Aprili29  2014  saa 10:31 AM
KWA UFUPI
  • Mboka na mwanamke huyo waliondoka kwenda kwenye zahanati hiyo kwa pi





Mbeya. Aprili 6, mwaka huu ni siku ambayo mkazi wa  Kijiji cha Kibanda wilayani Kyela, Mboka Mwakikagile (20) haitaisahau.
Ni siku ambayo aliibiwa mtoto mchanga wa kiume aliyekuwa na umri wa siku saba tu.
Akisimulia tukio hilo, Mboka anasema  alijifungua salama Machi 30 akiwa nyumbani kwa wazazi wake ambao ni  Lupalo Mwakikagile (90) na mkewe Nelly Kyusa (49).
 Anasema akiwa katika siku ya saba, alipigiwa simu na mzazi mwenzake (jina linahifadhiwa) kwamba  mama yake mkubwa atafika nyumbani kumwona mtoto.
Anasema baada muda mfupi mwanamke huyo  alifika kwa pikipiki akiwa na mkoba  uliokuwa na nguo za mtoto, sabuni na vifaa vingine.   “Baada ya kumkaribisha  na kusalimiana na wote , mwanamke huyo alimchukua mtoto na baadaye alinishauri twende  Zahanati  ya Njisi akatibiwe jicho ambalo lilikuwa linamsumbua kidogo,’’anasema.
Mboka na mwanamke huyo waliondoka kwenda kwenye zahanati hiyo kwa pikipiki na kwamba baada ya kufika hapo,  daktari aliwataka wanunue daftari  na mwanamke huyo alitoa Sh2,000 na kumtaka akanunue.
 ‘’Nilipokea fedha hizo na kumwachia mtoto pamoja na simu yangu wakati mimi nikielekea kununua daftari  kwenye duka lililo mbali na zahanati hiyo,’’ anasema.
Anasema mara baada ya kurudi dukani alishtuka kutomwona mwanamke na mtoto wake.
 Anaongeza kuwa  alimwomba daktari simu na kumpigia mzazi mwenzake ambaye alimjibu kwamba asiwe na wasiwasi kwani inawezekana alitoka  mara moja.
 ‘’Nilikwenda eneo la bodaboda na kuwauliza madereva kama walimwona mwanamke akiwa na mtoto. Walikiri kumwona akiwa na wasiwasi na kwamba alipanda pikipiki na kuondoa,’’ anasema.
 Anasema  baada ya kuambiwa hivyo, aliangua kilio jambo lililowafanya  majirani  wa eneo hilo kutaharuki na kufika kumpa pole.
Mboka anasema  alikwenda kutoa taarifa  Kituo cha Polisi Kasumulu , lakini cha ajabu alipofika alimkuta mzazi mwenzake akiwa kituoni hapo.
Chanzo:Mwananchi
Na Mjumbe Jr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top