Waziri mkuu nchini Korea Kusini
amejiuzulu kutokana na vile serikali yake ilivyolichukulia swala lote la
ferry iliozama siku kumi na moja zilizopita.
Chung Hong Won amesema kuwa kusalia afisini ni mzigo mkubwa kwake.
Bwana Chung alizomwa alipozitembelea
familia za waathiriwa waliotoweka katika ferry hiyo ya Sewol,baada ya
kuzama katika hali ya kutatanisha.
Takriban watu 200 wanadaiwa kufa maji
katika tukio hilo huku zaidi ya mamia wengine wakiwa hawajulikani
waliko,wengi wao wakiwa wanafunzi na walimu waliokuwa wakielekea katika
ziara ya shule.
Wapiga mbizi bado wanaendelea kuwasaka waathiriwa chini ya ferry hiyo iliozama.
Ripoti za awali zimedai kuwa watu wote wametolewa katika boti hiyo.
CHANZO BBC
Post a Comment