Unknown Unknown Author
Title: WOSIA WA MAMA:NIKIFIKIRIA KUSTAAFU KAZI MWANANGU... NINAPO WAONA WALIO STAAFU ! MOYO WANGU UNASHITUKA SANA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
   Pichani:Mama yangu a.k.a Mama Misana    Picha:Mama Yangu akisiitiza Jambo Leo ni Moja ya Siku Chache ambazo nime bahatika kuketi ...
   Pichani:Mama yangu a.k.a Mama Misana

   Picha:Mama Yangu akisiitiza Jambo

Leo ni Moja ya Siku Chache ambazo nime bahatika kuketi chini na Kuongea na Mama yangu huyu... Umekuwa ni Utaratibu wangu ninapo pata fursa kutenga muda wa kubadilishana Hikima na Wazazi wangu,ndugu na Jamaa.
Tume Zungumza mengi sana Lakini jambo kuu alilo nisisitiza Mama yangu ni kwamba "mwanangu jifunze kujiwekea Akiba yako na kuhakikisha unajifunza kubuni mradi unao weza kuwa na Tija kwako.
Unajua Tunapo kuwa Kazini Hii pesa ambayo kila siku Tuna Lalamika kuwa ni kiasi kidogo inatulemaza sana,hasa hii ya kila mwezi kuingiziwa Mshahara! Hii Inagharimu Watumishi wengi wa hii kada yetu(Walimu) na Baadhi ya Maasikari ambapo hujikuta mpaka wana Staafishwa hawana hata Vyumba viwili vya kuishi hasa ukizingatia Wengi wana ishi katika Nyumba za Serikari.Hapo Unapo peleka barua ya kumba kustaafishwa tu Wanakukatia Mshahara wako na kama ulizoea kuona Unaingiziwa Pesa Unaweza Shangaa Inapita hata miezi mitatu hujashughulikiwa Malipo yako ya Kustaafu.
Unapolipwa Pesa ile inakutana na orodha ya Madeni na Huna Nyumba,wapo wanao panga Lakini Suala la kupanga nyumba katika Umri wetu kama huu ni kujitukana na kujidharirisha na mwisho Mwenyenyumba ana weza kukufukuza kwani kama MUNGU akikupa Maisha marefu Unaweza ukaishi hata miaka Ishirini baada ya Kustaafu,Kama Hukujiwekeza Katika Rasirimali watu na Vitu Utaishije? Hapo ndipo mwanzo wa kugeuka omba omba na kuanza kuwa gumzo la kila unapo pita kwani Watu wata kuwa wana Sema "Yule naye eti amewahi kuwa Mwalimu";Jiulize kwanini wasiseme Huyu ni Mwalimu Mstaafu Mpaka Waseme eti amewahi kuwa mwalimu? Maanake hufanani na Walimu wenzako!
Mwanangu ninyi siku izi muna anza kazi mkiwa bado muna umri Mdogo na wengine Munabahatika muna anza kazi mkiwa na wazazi wanao weza kujitegemea na Munakuwa bado hamujajiingiza kwenye kuoa ama kupata watoto kabla,Hilo ni Suala Zuri kama mlivyo weza kuwa Hivyo Fanyeni jitihada sasa za kutengeneza Maisha ambayo mngetaka mje muya ishi baadaye,kwani leo muna nafasi lakini katika maisha huwa inafika kipindi Mtu anakua hana chaguo la kuamua aishi vipi ila anajikuta ndani ya mfumo wa maisha ambao haupendi aupitie.
Zaidi ya yote wengi mume ajiriwa mkiwa na Elimu ya Chuo,Hiyo ni Fursa kwenu kwani hata Mishahara yenu ipo juu ukilinganisha na tulivyo anza sisi enzi zetu.Kipato kilikuwa kidogo na fursa ya kupata elimu ilikuwa finyu sana,leo hii hata mimi nikitaka kujiendeleza katika fani yoyote ile naweza jiendeleza huku naendelea na kazi yangu kwani Vyuo vipo mpaka upenuni mwa nyumba zetu.Itumieni Elimu yenu kubwa vema na kwa busara,pia pesa mulizo anza nazo ninyi kama malipo ya mishahara zisi wafupishie maisha bali ziwe sehemu ya Baraka na Neema ndani ya maisha yenu;MUNGU awasaidie.
Tofauti kubwa nyingine iliyo jitokeza kwetu na ninyi ni kuwepo kwa Fursa za Kifedha nyingi zinazo weza zika kuwezesha ukajipatia Mkopo na Ukaweza kutekeleza kile unacho hitaji kwa wakati.Ukweli ni kwamba kama mutategemea Hicho kimshahara chenu tu ndio mkasema kita tosha kufanyia kila kitu utaishia kuitwa jina mwalimu tu Lakini Hakuna jambo ambalo jamii itakaa ijivunie Ualimu wako Lakini Ukitumia Vema Pesa hiyo Itakujengea Heshima kwani utafanya mambo ambayo yanaonekana kwa wakati.Ila pia Jihadharini sana na Hivyo vitaasisa Uchwara wengine wamewahi Panda Mbegu ili wavune lakini mpaka leo wameishia kulaghaiwa(DECCI),Pia yapo makampuni yanayo weza kukulaghai kwa Lugha tamu lakini mwisho wake wengi wame Ishia kudhulumiwa na kukatwa Mishahara yao bila Ukomo na Hakuna Walicho kifanya.Mifano tunayo na wengine hata wewe Unawajua! Jihadhari sana;Na unapo amua Kukopa kopa Mahari Salama na Ukope ukiwa na Lengo ambalo si Unaenda kuanza Bali utaliendeleza kutoka pale Ulipokuwa.Sio Unakopa ili Ujaribu kukwenda kuuza Ndizi Tukuyu kwa kutoka nazo Mwanjelwa Utakuwa umecheza pata potea na Utaendelea kukatwa deni na wale walio kukopesha.

Pia Mwanangu kama hii pesa tunayo pokea leo tunasema ndogo sana na haitoshi Jiulize siku usipokuja kupewa hata hii ndogo utaishi vipi? Kwahiyo mwanangu jiandae kuanzia Leo ili usije ukaanza kudharirika.
Mimi Nina Msikiliza kwa makini na kucheka anapo nisimulia maisha ya zamani na ya leo!

Huu nao ni wosia wa Mama! Wosia wa Mama kwa mwanae Hauishi! Kila anapo pata fursa ya kutoa ana Ongezea na kuongezea na Kuongeza.
Na kwasababu huu ni wosia wa Mzazi;Sina Budi niuhifadhi kwa ajili ya kuweka kumbukumbu Sahihi wa watakao kuja siku za usoni.Nisije nika anza kusema Laiti Ningejua!
Kwani Majuto ni Mjukuu.

Mama yangu Anapo waona watumishi wenzake wengine Walio Staafu wanavyo ishi MOYO WAKE UNA SHITUKA!
#@MUNGU AKUPE MAISHA MAREFU KWANI BADO TUTA HITAJI MALEZI YAKO!
Picha Na MJUMBE Sr(Nyumbani Hapa)

Elasto Mbella
Mlowo/Mbozi

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top