Unknown Unknown Author
Title: CWT:MSIMAMO WETU NI SERIKARI TATU!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
 Rais wa CWT Gratian Mukoba  Chama cha Walimu nchini (CWT), kimesisitiza kuwa msimamo wake ni muundo wa serikali tatu. Akizungumza...
 Rais wa CWT Gratian Mukoba

 Chama cha Walimu nchini (CWT), kimesisitiza kuwa msimamo wake ni muundo wa serikali tatu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Rais wa CWT, Gratian Mukoba, alisema Chama cha Walimu Tanzania mwishoni mwa mwaka jana kikiwa kama Taasisi Huru, kilikaa kama Baraza la Katiba na kuazimia juu ya Muundo wa Muungano wa Serikali tatu.
Alisema baada ya Mkutano Mkuu kupitisha kwa kauli moja Oktoba, mwaka jana, alipeleka maoni yao kwenye ofisi za Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kuyakabidhi.
“Tuliposikia rasimu ya pili imetoa maoni hayo, tuliridhika kuwa maoni yetu yamekubalika,” alisema.
Aidha, Mukoba alisema CWT kama zilivyo taasisi nyingine, kina wanachama wengi wenye mitazamo tofauti, lakini kikifikia makubaliano katika mambo ya msingi, lazima maoni ya taasisi yawekwe mbele, na maoni binafsi yahifadhiwe moyoni.
Alisema wanaamini katika Muungano wa kweli na kwamba haiwezekani mtu akaishi amefunga geti la nyumba yake na akiulizwa kwa nini huwa halifunguliwi akajibu kuwa anahofia mke wake ataondoka.
“Mke au mume anatakiwa kutoka na kurudi nyumbani bila kuwekewa shinikizo la kufungiwa geti,” alisema.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top