Unknown Unknown Author
Title: KOCHA MPYA "LITIMBE" KUINOA TIMU YA KIJIJI,AMANI,LUDEWA! UHABA WA VIFAA VYA MAZOEZI WATAJWA KAMA KIKWAZO!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
 Baadhi ya Wachezaji wakikatiza Mitaa ya Kijijini Amani;Wakitokea Kutafuta Pumzi nje ya Kijiji Vijana Wakiwa Uwanjani,Wakifuatiliwa kwa...
 Baadhi ya Wachezaji wakikatiza Mitaa ya Kijijini Amani;Wakitokea Kutafuta Pumzi nje ya Kijiji
Vijana Wakiwa Uwanjani,Wakifuatiliwa kwa Karibu sana na Kocha wao Mpya


Pamoja na Kibaridi HIKI cha Njombe;Vijana wana Pasha wakiwa Vifua wazi na Jasho Likiwatiririka!

Mchezaji wa Timu ya Amani aliye Julikana kwa Jina Moja tu la Mwalimu Mligo akionjeshwa Mikunjo ya Litembe Uwanjani!
Baadhi ya Wachezaji wakimsikiliza Kocha wao kwa Makini
Baadhi ya Viongozi wa Kijiji cha Amani walio ombwa ili waje watoe Baraka zao kwa Vijana;Ili wawa Ruhusu wafanye Mazoezi na Wasishiriki kwenye shughuli za maendeleo ya kijiji.

Kocha Mpya wa Timu ya Amani,akitoa maelekezo kwa Vijana wake.

Kamera Yetu iliyo piga kambi Tarafa ya Liganga ili bahatika Kufika Eneo la Tukio ambalo Vijana walikuwa wana Fanyia Mazoezi yao wakijinoa tiari kukabiliana na Mechi zijazo mbele yao!

Mdau wa MJUMBE BLOG Alibahatika kusikiliza na kutazama Maombi ya kocha wa Timu hiyo ambayo ilikua kama ime potea na imeanza kurudi kwa Kishindo mara baada ya Kocha anaye jitolea zaidi anaye julikana kama Litimbe kuwa unganisha na Kuanza kurudisha Nidhamu kwanza kwa Mchezaji mmoja mmoja na kisha kuwapa maelekezo na Mazoezi Bora zaidi!
Akiongea Mbele ya Baadhi ya Viongozi wa Kijiji cha Amani,Bwana Litimbe aliezea jinsi alivyo kabiliana na Mpasuko alio ukuta awali na Mipango aliyo jiwekea kwa Timu hiyo na Maono yake.Hata hivyo alizitaja baadhi ya changa moto zinazo mkabili katika shughuli hiyo kwa kubainisha kuwa bado kuna Uhaba wa Vifaa vya kufanyia mazoezi,badala ya pia au koni wanatumia Nguo au makopo! Jezi pia Limekuwa Tatizo kwani wachezaji au Timu haina Jezi zaidi ya Zile alizo zitoa Mhe.Deo Filikunjombe mwaka jana! Pia Hakuna Vifaa vya vya huduma ya kwanza.

Wadau mbali mbali wa Michezo kijijini Hapo ukiwepo Uongozi wa Kijiji Ulionekana kuunga mkono Wazo la Mwalimu huyo ambapo Uliahidi Kwasiriana na Serikari ya kijiji cha Amani ili ilitambue zoezi hilo na iwaondoe vijana hao Katika orodha ya Kuchangia Michango ya Maendeleo!
Wadau hao pia wali ahidi kutafuta wafadhiri wa Timu na kushawishi wadau wa Kandanda wajitolee ili kununua vifaa vya Michezo vya Timu Husika.

Mwalimu huyo aliye hakikishia Timu yake na Mashabiki wake ushindi na kusogea mbele kimichezo katika Wilaya yake;Aliendelea Kutoa matumaini kwa Wadau wa Mpira na Mshabiki wa Timu Yake.
Alisisitiza zaidi suala la Nidhamu na Uvumilivu kwa wachezaji pia aligusia suala la Umoja kwani ndiyo siri ya Mafanikio,katika Mapambano yote yaliyo mbelle yao.

MJUMBE Sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top