"Huwezi
kusimama hapa mtu na macho yakakutoka halafu unaanza kulizungumzia taifa
lingine ambalo siyo lako, hivi unatoa wapi ujasiri huo au wanakulipa,"
alihoji Membe na kuongeza.
Wakati
Bunge likipitisha bajeti ya makadirio ya matumizi Sh191.91 bilioni ya
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka wa fedha
2014/15 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard
Membe, alitumia nafasi hiyo 'kumchana' Ezekiel Wenje na kusema kuwa
anatumiwa na mataifa ya nje.
Mbali na
hivyo aliwaita watu wanaotoa kauli za uchonganishi kuwa ni wapumbavu na
akataka waache tabia za kipumbavu kwani hawatavumiliwa hata kidogo.
Membe
alitoa kauli hiyo jana jioni wakati akitoa majumuisho katika michango ya
wabunge kwenye hotuba ya mapato na makadirio ya wizara hiyo kwa mwaka
2014/15
Wenje
ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa jana asubuhi katika hotuba yake, alimshambulia Membe kuwa ni
waziri mzigo ambaye hajui wajibu wake.
Sakata hilo liliibuliwa kwenye uhusiano baina ya Tanzania na nchi ya Rwanda ambalo Wenje alilizungumzia zaidi.
Akijibu
hoja hizo Membe, alisema: "Kwanza nikubaliane na kauli ya wabunge wengi
kuwa uhusiano wa Tanzania na Rwanda siyo mzuri kwani kila upande
haumuamini mwenzake," aliema Membe.
Alisema
kinachowaumiza pande zote ni kuwa kila upande unapozungumza na mahasimu
wa mwenzake, wanahisi kuwa anataka kuipindua Serikali yao hivyo bado
hawajakubaliana kwa jambo lolote lakini akasema yote yatakwisha salama.
"Huwezi
kusimama hapa mtu na macho yakakutoka halafu unaanza kulizungumzia taifa
lingine ambalo siyo lako, hivi unatoa wapi ujasiri huo au
wanakulipa,"alihoji Membe na kuongeza.
"..Mimi
naweka rehani uwaziri wangu hapa kwamba ukileta vielelezo kamili mimi
nitakuwa tayari kuachia nafasi yangu, je na wewe nikitoa vielelezo
utakuwa tayari kuwajibika."
Alimtaja
Wenje kwa jina kuwa alichokifanya hakifai kuwa alitoa kauli ambayo siyo
nzuri kwa siri za taifa na akasema mtu kama huyo akipata nafasi hata
kama nchi itakuwa vitani, yuko tayari kutoa siri.
Aliyataja
makundi ya ya M23 kuwa ni moja ya kundi ambalo linaundwa na
Banyamulenge waliokuwa chini ya Roral Nkunda pamoja na kundi la FDRA
ambalo liliua watu wengi kwamba linaundwa na Wahutu bila ya ubishi.
Membe
alimpongeza mbunge Alli Keissy kuwa alichokizungumza jana asubuhi kuhusu
Rwanda na DRC Kongo ni sahihi na ndiyo maana alimshangilia kwa nguvu
zote.
Chanzo: Mwananchi
@Sr
Post a Comment