Unknown Unknown Author
Title: MJUE MSOMI HUYU ALIYE TOA KAULI NZITO KWA VIJANA;MIMI SIKUSOMA ILI NIAJIRIWE! ...MATUMIZI YANGU YA KAWAIDA NI ZAIDI YA MSHAHARA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Yassir Mchumi Na Kiongozi   Wakati vijana wenzangu wakizunguka na bahash za kuomba ajira mtaani...Na mimi nazunguka kuomb...
Wakati vijana wenzangu wakizunguka na bahash za kuomba ajira mtaani...Na mimi nazunguka kuomba ushauri toka kwa wataalamu wa kilimo.

Nilipo maliza chuo kikuu,dhana yangu ya kwanza kabisa niliyokuwa nimeijenga kichwani mwangu ilikuwa ni hii: "MIMI SIKUSOMA ILI NIAJILIWE"

Nilienda shule kusoma ili niongeze utambuzi ni fute ujinga na nipanue uwezo wa kuzitambua fursa zaidi

Dhana yangu hii ilikuwa ni ngumu sana kwa mama yangu kuilewa na kunielewa binafsi,nahisi alihisi kama nimechangnyikiwa hivi

Nilimuona Aunty yangu akikazna na magazeti mengi sana mara daily news,Citizen,Sunday news na mengine.....sikupenda kumkatisha tamaa nilizichukua zile gazeti na kuzisoma na vile visehem vya vacancy wala kwangu sikuvipa vipa umbele sana.....Sikusoma ili nije kuajiliwa

Sababu za kunifanya niwaze hivyo zilikuwa ni nyingi sana

1.Niliona matumizi yangu ya kawaida ni zaidi ya mshahara ambao ningelipwa kwa mwezi

2.Upatikanaji wa Ajira ulibeba njia chafu nyingi,nilijiuliza kwa nini nisome kwa shida,nitafute kazi kwa shida,mshahara mdogo tena ntaishi kwa shida niliona hizi shida zote za nini?

Nilikuwa natambua kiu na kilio cha mama yangu cha kunitaka nitafute kazi mara kwa mar, nilijua fraha kwa mama ni pale mtoto anapo soma na akamaliza na kupata kazi nililitambua sana....lakini bado mimi sikusoma ili niajiliwe,

Kazi ya kunielewa mama yangu haikuwa kazi rahisi hata kidogo ,nilijua mama angu kama wazazi wengine alipenda mwanae apendeze avae tai na atoke offcine na pengine afanye kazi pale BOT niliziona ndoto zake na hiyo ndo faraja na furaha kwa wazazi wengi na ili apate kuhadithiana huko na wenzake mwanangu anafanya kazi BOT.....Lakini mimi bado sikusoma ili niajiliwe kama ni ajira ije kama fursa lakini sio lengo kubwa hasa lilokuwa mbele yangu

Nilijua kuvaa na kupendeza hakutaninunulia kiwanja,kuvaa na kupendeza hakutaninulia nyumba, pengine hakutanilishia mke wangu na vinginevo...hivyo swala la kuvaa na kupendeza kwangu halikuwa kipa umbele cha kwanza au cha pili pengine ni cha mwisho kabisa

Nilijua kazi za kuajiliwa ili uwe na maisha kwa maana ya maisha ni lazima uchepuke kazini...ni lazima uumize wananchi...ni lazima ukwibe huu ndo ukweli na niliona na kwa nini hayo ndo yawe maisha yangu? Hivo nilitizama kwa fikra tofauti

Wazazi wetu hawapendi tufanye kazi za kujichafua tukishamaliza kusoma,hawapendi tufanye kazi za nguvu na mda mwingi hata sisi wenyewe sharoboys na sharobabys hatupendi any way ni marefu

Mimi ni rafiki sana kwa sasa na wataalumu wa kilimo,ni rafiki sana na wataalmu kutoka pale SUA

Tunapo kutana wao wana taalumu kuhusu udongo hivyo wao wataniambia kuhusu udongo mimi ntawambia kuhusu dynamic population

Objective function yetu ni tunatapateje fursa?

SUA ana taaluma ya udongo lakini hana taalumu kuhusu tabia za soko na tabia za fedha na mzunguko wake,hana taalifa sahihi kuhusu population dynamic

Tunapo kutana mazungmzo yetu lazima yalenge pale katika kila mtu asicho kijua

Mfn mimi namwambia after 25ys to come Tanzania itakuwa na population isiyo pungua watu 80 M na Dar es salaam tu itakuwa na watu zaidi ya 20 M

Tunayo Aridhi tunao watu kwetu kwetu tiyari ni fursa

Tunacho takiwa kukifanya ni kukaa na kutafakari sasa Populationa hii na aridhi hii kwa elimu zetu kwetu ni fursa kiasi gani?

Tathimini ndogo uzalishaji wa bibi zetu huko kijijini hawezi tena kutosheleza soko la ndani after ten years to come,,,,,Tufanye nini? Je vikwazo ni vipi? Na je tunachomoka?

Kilimo kwa Tanzania bado ni frsa nzuri sana ambayo kwangu nadhani haitaji barua za maombi baada ya kuwa umemaliza masomo yako

55% Aridhi ya Tanzania haijaguswa na shughuri zozote za kilimo au makazi ya binadamu, maana yake aridhi hii bado ni tupu leo 13% inamilikuwa na wawekezaji ambao wanatoka nje kuwekeza kwetu

Tunaweza kutafuta visingizo vingi sana tukisema masoko na vingivo lakini ukweli ni kwamba hata soko la ndani kwa baadhi ya kilimo chetu hakijajitosheleza kutulisha ,sasa hapo tunataka soko gani?

Mimi bado naamimi na nina imani kubwa bado kilimo Tanzania ni fursa nzuri,na nnaweza kulima nkiwa nimevaa suti ni just mipango tu

Aridhi tunayo ya kutosha sana,aridhi yetu bado ni rutuba

Salam kwa Mh Shukuru Kawabwa ile mapinga na pwani ntalima sana

Kwangu rasilimali kubwa ni hawa wataalamu,huwezi kufanya kilimo kama kujifurahisha, unafanya kilimo kidogo na chenye tija na faida kubwa

Kwa sasa mama yangu kwa mbali anaanza kunielewa nilikuwa namanisha nini

Huyu ni mtaalumu wangu ambaye ni consultant wa kilimo anafanya kazi na shirika kubwa tu la kilimo cha mazao yote Bolton Tanzania Ltd ambalo makao makuu yake yapo pale mikocheni karibu na mwenge barabara ya kuelekea kilipo kiwanda cha Cocacola, hata wewe ukimuhitaji unamchangia mafuta anakuja kwako pia,ukimuhitaji tuwasiliane

Lengo langu la badae ni kuilisha Dsm Nzima mboga mboga za aina zote kuanzia Nyanya,Vitunguu,Kabichi,Pilipili hoho, nk
 
MJUMBE SR

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top