Kenya inaendelea kufanya vizuri katika mashindano ya kukimbia baada
ya timu za taifa za kukimbia kwa wanawake na wanaume kuvunja rekodi
zilizokuwepo katika mashindano hayo ya kupokezana vijit kidunia.
Rekodi ya mbio za mita 1500 ya wanawake ilivunjwa na Wakenya Mercy Cherono, Faith Kipyegon, Irene Jelagat na Hellen Obiri walipotumia muda wa dakika 16:33.58 zaidi ya sekunde 32 ndani ya rekodi ya awali.
Kwa upande wa timu ya wanaume pia imevunja rekodi baada ya kukimbia katika mbio hizo za kupokezana vijiti na kumaliza katika dakika 14:22.22 ikiongozwa na Collins Cheboi, Silas Kiplagat, James Magut pamoja na Asbel Kiprop.
Ethiopia ilimaliza katika nafasi ya pili kwa kukimbia ndani ya muda wa dakika 14:41.22 .
Licha ya kushindwa matokeo hayo yaliipa Ethiopia rekodi mpya ya kitaifa.
Marekani ilifunga orodha ya tatu bora ikiongozwa na Leonel Manzan ambaye aliandikisha rekodi mpya ya kitaifa ya dakika 14:40.80.
Rekodi Nyengine iliyowekwa ni mbio za mita 200 kupokezana vijiti ambapo wajamaicaNickel Ashmeade, Warren Weir, Jermaine Brown na Yohan Blake.
Wanne hao waliandikisha muda wa dakika moja 1:18.63.Rekodi ya awali ya dakika 1:18:68 iliwekwa na Marekani miaka 20 iliyopita.
Shirikisho la riadha duniani IAAF liliwatuza washindi wote wa rekodi mpya dola elfu hamsini kwa juhudi zao.
MJUMBE Sr

Post a Comment