Unknown Unknown Author
Title: MTATIRO NA KITENDAWILI CHA KIGAMBONI!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Julius Mtatiro KITENDAWILI CHA KIGAMBONI - CCM WAPIGA KELELE WATAUFYATA TU! Jana nilishuhudia sarakasi za wabunge dhidi ya waziri wa ...
Julius Mtatiro

KITENDAWILI CHA KIGAMBONI - CCM WAPIGA KELELE WATAUFYATA TU!
Jana nilishuhudia sarakasi za wabunge dhidi ya waziri wa Ardhi Mhe. Tibaijuka. Wengi wa wabunge ambao walitishia kutoa shilingi ni wale wa CCM na huku waziri yeye akidai kazi yake ni ya kitaalamu na kwamba anatimiza wajibu.
Hata hivyo kwa uzoefu wa utawala wa nchi yetu, suala lile sasa imekubalika litizamwe upya, wabunge wenye ushawishi na wanaohusika katika jambo hilo au linagusa maslahi yao wataungana na madiwani wa TEMEKE na serikali ili kulitizama upya.
Kwa bahati mbaya najua litachukua sura mpya, "Combination" ya CAUCAS iliyotajwa hapo itakuwa DORMINATED na CCM na mwisho wa siku wale wengine watakuwa kama waalikwa kwenye mkutano wa maamuzi wa CCM. Baadaye watatishwa ati suala hilo litahatarisha ushindi wa CCM 2015 na kutishia uwepo wao madarakani na kwamba sasa wanapaswa kusimama kidete kuungana na POROJO za waziri na PROPAGANDA za serikali, masikini watakubali, KWA KUHOFIA chama chao kuonekana kigeugeu 2015 na eti kile kinachoitwa kutekeleza ahadi ya "KIDUMU CHAMA"!
Watakapotoka katika hicho wanachokiita "SERIKALI KULITIZAMA SUALA LA KIGAMBONI UPYA", mtaniambia...watakuwa wameshaufyata, KIMYAA....Na ni kawaida ya serikali yetu kuchezea viongozi ambao wako sokoni. Huko kwenye kulitizama upya kila mpiga kelele atapewa ekari zake 20 na kuahidiwa kuletewa mwekezaji ambaye atasimamia ujenzi, KELELE ZA WANANCHI WASHIRIKISHWE zitakufa ghafla, Kelele mpya zitakazoanza zitasema "WABUNGE WAMESHIRIKISHWA NA WAO NDO WAWAKILISHI WA WANANCHI NA KWA HIYO SAUTI YA WANANCHI IMESIKIKA!". Nchi yenye nyimbo na mashairi ya kutosha. Lahaula!!!!!!! Naipenda Tanzania nchi yangu.
Asubuhi njema.
J. - DSM.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top