MOTO WATEKETEZA LORI LA MAFUTA, MBEYA.;
Lori la kusafirisha mafuta likiwa na shehena kubwa ya mafuta aina ya Diesel lita 35,000, limeteketea kwa moto baada ya kupata ajali ya kugongwa na Lori lingine katika eneo la Igurusi Wilayani Mbarali, Mbeya.
Baadhi ya wananchi ambao wameshuhudia ajali hiyo, wameitaka Serikali kuwalazimisha wamiliki wa malori kuhakikisha magari yao yanakuwa na Madereva wa akiba kwa kuwa wanaamini kuwa ajali hiyo imesababishwa na Dereva wa Lori mojawapo kusinzia wakati akiendesha Gari kutokana na uchovu wa safari ndefu.
#EATV#
MJUMBE Sr
Post a Comment