Albert G. Sengo kutoka Mwanza anaripoti Mmisionari Simon Nyirani
Mhagama wa Shirika la Mt. Kalorilwanga ambaye anasambaza ujumbe kuhusu
hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere kuwa Mtakatifu wa 21 tangu
tarehe 20/03/2013.
Picha ya
mwisho ya Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere aliyopiga
kijijini kwake Butiama kabla ya kwenda kupata matibabu nchini Uingereza
ambapo alifia katika Hospitali ya Mt. Thomas.
Wakati yote haya yakifanyika kutoka
nchini Uganda: Rais Yoweri Museveni, amesema kiongozi bora ni yule
anayefuata maagizo ya Mungu na kuwatumikia binadamu wote kwa usawa na
haki.Rais Museveni aliyasema hayo Tarehe moja mwezi June, wakati wa ibada ya kuombea mchakato wa kumfanya Marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuwa mwenyeheri na hatimaye kutangazwa mtakatifu
Picha ya
mchoro wa Mtakatifu Charles Lwanga aliyemtangaza Hayati Baba wa Taifa
kuwa Mtakatifu wa 21 ambapo alisema hata kwenye maandiko matakatifu ya
Biblia kuna mistari inayomtaka binadamu ampende binadamu mwenzake kama
anavyojipenda yeye.
Rais
Museveni alisema anatarajia kupeleka ushahidi kwa Papa Benedict kwamba
Mwalimu Nyerere ana sifa za kutangazwa kuwa mtakatifu kwa sababu alimtii
Mungu na kuwatumikia binadamu.
Mmisionari
Simon Nyirani Mhagama wa Shirika la Mt. Kalorilwanga ambaye anasambaza
ujumbe kuhusu Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere kuwa
Mtakatifu wa 21 akiwa katika picha ya pamoja na watoto waliotembelea
kaburi la Baba wa Taifa Butiama mkoani Mara.
Kufuatia hatua hiyo ya kwenda Roma
kutoa ushahidi, Rais Museveni amesema katika maadhimisho ya kuombea
mchakato wa Mwalimu kuwa Mtakatifu yatakayofanyika mwakani, ameahidi
kuwaita maraisi wote waliowahi kufanya kazi na Mwalimu Nyerere ili
kuuthibitishia ulimwengu kuwa Marehemu Baba wa Taifa ameweza kuwa
unganisha Waafrika.Alifafanua kuwa Mwalimu ametoa mchango mkubwa wa ukombozi kwa nchi za Msumbiji, Zambia, Zimbabwe, Namibia, Angola, Afrika Kusini, Uganda na Tanzania yenyewe. Hivyo kuja kwa viongozi hao kushiriki ibada hii itakuwa Baraka kubwa.
Kwa kanisa katoliki utakatifu ni hatua ya tatu baada ya hatua ya kwanza ambayo ni Mtumishi wa Mungu,hatua ya pili ni Mwenye Heri na hatua ya tatu ni Mtakatifu ambapo miujiza mbalimbali pamoja na taarifa hukusanywa kupelekwa makao makuu ya Kanisa hilo.
Na:Awadh Ibrahim.
MJUMBE Sr
Post a Comment