CCM epukeni kutumia misiba ya
Watanzania kisiasa!
Nimestushwa na nguvu kubwa ya
kipropaganda inayofanywa na "ccm"
kupitia vyombo vya habari ati
Chadema haijashiriki msiba wa mjumbe
wake wa kamati kuu Marehemu Bi
Shida Salum na Mama Mzazi wa Mh
Zitto Kabwe.
Hii ni aibu na hatari kwa chama
tawala nchini kufanya ulaghai wake
hata kwenye msiba wa mtanzania,
Chadema imeshiriki kumuuguza Bi
Shida Salum akiwa hajazidiwa,
Mwenyekiti wa Chama Mh Freeman
Mbowe alikuwa ni kiongozi wa kisiasa
wa kwanza kwenda kumjulia hali na
kutoa msaada wa matibabu kwa
niaba ya chama,
Pia alipozidiwa na kufikishwa
Muhimbili, bado Chadema iliendelea
kuwa sehemu ya wanaomuuguza Bi
Shida Salum, ambapo viongozi wa juu,
na wabunge walifika kumtaka hali
pale Muhimbili, huku shughuli za
kichama zikiwa zinaendelea (ziara ya
Ukawa) nchini.
Taarifa ya msiba wa mama yetu na
Mjumbe wa kamati kuu, zilitukia
wakati viongozi wa juu wakiwa
ziarani ambapo Dr Slaa akiwa Singida
na Mh Mbowe akiwa Arusha,
kutokana na mazingira waliyokuwepo
kijiografia kuwa ngumu kuwahi
mazishi kule Kigoma,
Hivyo Chama Makao makuu kikateua
ujumbe utakao wakilisha chama
msibani, ambapo aliteuliwa Waziri wa
Mambo ya Nje/Mjumbe wa Kamati
Kuu na Mbunge wa Nyamagana Mh
Wenje kuongoza ujumbe huo.
Ujumbe na Wabunge walioenda
kumzika Bi. Shida Salum ni
Alfi,Wenje, Mdee, Lucy, Mukya,
Muhonga,
Sabrena,Matiko, Anna mallac,
Masishanga,
Raya, Anton komu na wengine wengi.
Sasa binafsi najiuliza, hivi ccm
hawana utu wala aibu kiasi hiki
kutumia msiba wa Bi Salum
kujinusuru kisiasa??
Jana Kada Mashuhuri wa Ccm
aliyewahi kushika nyadhifa za juu
kabisa na ambae kwa sasa ni Mbunge
Mh Ritha Mlaki amefiwa na Mama
yake mzazi na msiba umesafirishwa
toka Dar kwenda Moshi, lakini hakuna
kiongozi wa juu aliyefika hata kumpa
pole tu mh Mlaki, sio Nape, Mwigulu,
Kinana wala Jk. Huenda hawakupata
taarifa kwakuwa walikuwa bize
kwenye propaganda za msiba wa Bi
Shida Salum.
Binafsi ninalaani sana kitendo hiki
walichokifanya ccm, huu sio uungwa
wala utu, na sio asili ya siasa za
Tanzania kabisa.
"Kuna watu wasipokuelewa maneno na
matendo yako, mshukuru Jah, wewe
bado unafikra chanya, wakianza
kukuelewa jichunguze ni wapi
umeanguka maana umeanza kuwaza
kama wao"
by Yericko Nyerere
nguvu ya umbea na ushankunaku wa kipuuzi wanayotumia wangeitumia kuhoji
alikofia Balali ingewafaa sana!! Msiba sio sehemu ya mbwembwe za
kisiasa... kwamba ubebe makamera na waandishi ili tu uonekane ulikuwepo.
Chadema sio Mbowe na Dr Slaa pekee.. wabunge na viongozi walioenda
Kigoma ni watu na wamewakilisha taasisi pia.
MJUMBE sr
Home
»
»Unlabelled
» YERIKO NYERERE:CCM EPUKENI KUTUMIA MISIBA YA WATANZANIA KISIASA!
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment