Unknown Unknown Author
Title: KODI YA PAYE YASHUKA HADI ASILIMIA 12!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
...


Bajeti ya mwaka 2014/15 imewakumbuka wafanyakazi, baada ya serikali kupunguza kiwango cha kodi ya mishahara (PAYE) kutoka asilimia 13 hadi asilimia 12.
Waziri wa Fedha, Saada Salum Mkuya, alitangaza uamuzi huo jana wakati akiwasilisha bungeni bajeti na kufafanua kuwa uamuzi huo unalenga katika kutoa unafuu wa kodi kwa wafanyakazi.
Mkuya aliliambia Bunge kuwa pia, Serikali inaangalia uwezekano wa kupunguza kiwango hicho hatua kwa hatua ili kuwapa unafuu wafanyakazi.
Pamoja na hatua hiyo, hakuna uhakika kama itawanufaisha wafanyakazi kwa kiwango kikubwa kwani kodi hiyo iliposhushwa mwaka 2012 mfanyakazi anayelipwa mshahara wa Sh. milioni moja alijikuta mshahara wake ukiongezeka kwa Sh. 5,000 kwa mwezi.
Serikali pia imetangaza kuwa itaongeza kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa serikali.
 
 NIPASHE

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top